Rushwa

Maafisa 53 wa serikali wapo kortini kujibu tuhuma za ufisadi-DPP

DPP Norrdin Haji amemkabidhi rais Uhuru Kenyatta ripoti hiyi katika Ikulu ya Nairobi

Muhtasari

 

  •  Baadhi ya magavana na magavana wa zamani walioshtakiwa kwa ufisadi  wamezuiwa  kurejea katika afisi zao .
  •  Kulingana na ripoti hiyo wabunge saba ,mawaziri saba  na makatibu wa wizara  pia walishtakiwa kwa makosa yanayohusiana na ufisadi .
  • Haji katika ripoi yake hiyo ya kila mwaka amesema ukosefu wa usimamizi mzuri wa rekodi  ndio changamoto kubwa kwa afisi ya ODPP .

 

 

Ni kesi 53 pekee zinazowahusu maafisa wa serikali ambazo zimewasilishwa kortini  kati ya mwaka wa 2017 na 2020 .

  Hilo limefichuliwa  na Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji kupita ripoti maalum aliotoa  siku ya jumanne .

  DPP Norrdin Haji amemkabidhi rais Uhuru Kenyatta ripoti hiyi katika Ikulu ya Nairobi .

 Kwa mujibu wa ripoti hiyo ,wakurugenzi na maafisa wakuu 22 wamefikishwa mahakamani wakifuatwa na magavana 11 na maafisa wakuu wa serikali za kaunti .

 Baadhi ya magavana na magavana wa zamani walioshtakiwa kwa ufisadi  wamezuiwa  kurejea katika afisi zao .

 Miongoni mwao ni  Ferdinand Waititu (Kiambu),  Moses Lenolkulal (Samburu)  na Mike Sonko (Nairobi),  ambao wote wanakabiliwa na makosa ya uhalifu wa kiuchumi na kutumia vibaya maamlaka ya afisi zao .

  Takriban magavana  tisa wapo  chini ya uchunguzi wa EACC kuhusiana na tuhuma za ufisadi .

  Magavana hao ni ; s Okoth Obado wa Migori , Granton Samboja (Taita Taveta), Muthomi Njuki (Tharaka Nithi), Mwangi wa Iria (Murang’a), Charity Ngilu (Kitui), Mohamud Ali (Marsabit), Alex Tolgos (Elgeyo Marakwet)  na  Alfred Mutua (Machakos). 

 Kulingana na ripoti hiyo wabunge saba ,mawaziri saba  na makatibu wa wizara  pia walishtakiwa kwa makosa yanayohusiana na ufisadi .

 Wakilishi watano wa kaunti na naibu   kamishna mmoja wa kauti pia ni miongoni mwa waliosajiliwa mahakamani kwa kesi zinazohusiana na ufisadi .

Haji katika ripoi yake hiyo ya kila mwaka amesema ukosefu wa usimamizi mzuri wa rekodi  ndio changamoto kubwa kwa afisi ya ODPP .

 Hatua hiyo inafanya kuwa vigumu kukusanya maelezo kuhusu kesi mpya na zile ambazo zinaendelea .