Corona

17 wafariki huku 1459 wakipatikana na Corona

wagonjwa 59 wapo katika kitengo cha ICU

Muhtasari

 

  •  Kutoka visa hivyi 1,419 ni wakenya ilhali 40 ni raia wa kigeni .835 ni wanaume  huku wanawake wakiwa 624 .
  • Leo wagonjwa 780 wamepona  na kufikisha 50,658 idadi ya watu waliopona corona

 

Mutahi Kagwe
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe Mutahi Kagwe

 

 Watu 1,459 wamepatikana na virusi vya corona baada ya sampuli 10,146 kupimwa katika saa 24 zilizopita  na kufikisha visa vya ugonjwa huo nchini kuwa 74,145 huku  jumla ya sampuli zilizopimwa ikifika 815,0404.

 Kutoka visa hivyi 1,419 ni wakenya ilhali 40 ni raia wa kigeni .835 ni wanaume  huku wanawake wakiwa 624 .

 Leo wagonjwa 780 wamepona  na kufikisha 50,658 idadi ya watu waliopona corona .Hata hivyo watu 17 wameaga dunia na kufikisha 1330 idadi ya walioangamizwa na virusi hivyo . wagonjwa 1,116 wamelazwa katika hospitali mbali mbali huku 6,232 wakiwa chini ya  mpango wa utunzi wa nyumbani .wagonjwa 59 wapo katika kitengo cha ICU