Uchaguzi Nairobi

Thirdway Alliance chamuidhinisha Miguna kuwania ugavana Nairobi

Miguna wiki jana alitangaza nia ya kuwania kiti hicho

Muhtasari

 

  •  Hatua hiyo imejiri wiki moja baada ya Miguna kutangaza kwamba atagombea kiti hicho  baada ya IEBC kutangaza tarehe ya uchaguzi mdogo .
  •  Kupitia taarifa mwenyekiti wa Thirdway Alliance  Miruru Waweru amesema Miguna ndioye mgombeaji bora kulirejeshea hadhi jiji la Nairobi .

 

Miguna Miguna

 Chama cha Thirdway Alliance kimemzindua wakili  Miguna Miguna  kama mgombeaji wake wa ugavana katika uchaguzi mdogo utakaofanywa Nairobi .

 Hatua hiyo imejiri wiki moja baada ya Miguna kutangaza kwamba atagombea kiti hicho  baada ya IEBC kutangaza tarehe ya uchaguzi mdogo .

 Kupitia taarifa mwenyekiti wa Thirdway Alliance  Miruru Waweru amesema Miguna ndioye mgombeaji bora kulirejeshea hadhi jiji la Nairobi .

Wawru amesema Miguna ndiye chaguo bora kwa wakaazi wa  jiji kwani uongozi wake utakuwa  wa kuligeuza jiji na kuboresha utoaji wa huduma  na kuangamiza ufisadi .