- Mukhisa aliongeza , " Watu hawafai kutuambia mbona wanataka kuwa rais bali wanafaa kutuambia sababu za kutaka uongozi’
- Kituyi amesema anakamilisha muda wake kama mkuu wa UNCTAD na atarejea nchini kwa kampeini kabambe za kuingia Ikulu .
Mkuu wa shirika la UNCTAD Mukhisa Kituyi ametangaza kwamba atawania urais mwaka wa 2022
Akizungumza katika ngome yake ya Bungoma siku ya jumamosi baada ya kukutana na kundi la watalaam kutoka eneo hilo Kituyi amesema analenga kuwania kiti hicho kwa sababu taifa kwa sasa lina ‘pengo la uongozi’ kwa ajili ya jitihada za kumriti trais Uhuru Kenyatta mabaye muhula wake wa pili utakaribia kufika tamati .
“ Kila changamoto ni fursa kwetu …changamoto kwetu ni kwamba tuna idadi kubwa ya watu bila uongozi na ni wakati wetu kuongoza’ amesema
Mukhisa aliongeza , " Watu hawafai kutuambia mbona wanataka kuwa rais bali wanafaa kutuambia sababu za kutaka uongozi’
Kituyi amesema anakamilisha muda wake kama mkuu wa UNCTAD na atarejea nchini kwa kampeini kabambe za kuingia Ikulu .
Kuhusu uongozi wa jamii ya Waluhya Kituyi amesemajamii hiyo haijakuwa kiongozi kwa muda mrefu na ndio kwa sababu viongozi wengi wamejaribu kuleta umoja wa jamii hiyo bila mafanikio .
Kituyi amekuwa katibu mkuu wa UNCTAND tangu septemba mwaka wa 2013 na aliwahi kuwa waziri wa biashara na viwanda kuanzia 2002 hadi 2007
Awali alihudumu kama mbunge wa Kimilili kabla ya kupoteza kiti hicho kwa mbunge wa sasa wa Tongaren Eseli Simiyu baada ya eneo bunge la kimilili kugawanywa mwaka wa 2007 .