- Sonko alidai kwamba yeye ,Kibicho na maafisa wengine serikalini walinunua magari na kuyachoma mwaka wa 2017 na kisha kukilaumu chama cha ODM kwa ghasia hizo.
- Alizungumza katika eneo la Dagoretti katika hafla ambayo naibu wa rais William Ruto alihudhuria
Polisi wamemuagiza gavana wa zamani wa Nairobi ajiwasilishe ili kuhojiwa kuhusu madai yake kwamba yeye na maafisa wengine wa serikali walipanga na kutekeleza ghasia wakati wa uchaguzi mwaka wa 2017 .
Sonko anafaa kujiwasilisha kwa maafgisa wa DCI katika makao makuu ya idara hiyo jumatatu ijayo . Agizo hilo kwa Sonko limetolewa na mkuu wa uhalifu mkuu Obadia Kuria . Hii ni baada ya katibu wa kudumu wa wizara ya usalama wa ndani Karanja Kibicho kulalamika kwa polisi kwamba Sonko alikiri kutekeleza uhalifu na anafaa kuchukuliwa hatua .
Sonko alidai kwamba yeye ,Kibicho na maafisa wengine serikalini walinunua magari na kuyachoma mwaka wa 2017 na kisha kukilaumu chama cha ODM kwa ghasia hizo.
Alizungumza katika eneo la Dagoretti katika hafla ambayo naibu wa rais William Ruto alihudhuria . Kibicho amekana madai hayo na kupa kuhakikisha kwamba Sonko analipia kwa uhalifu aliotekeleza .
Kibicho alijondoa lawamani kuhusu madai hayo na kumshtumu Sonko kwa kumchafulia jina . Kibicho pia amesema atatafuta usaidizi wa kisheria na mahakama kuhusu madai aliotoa Sonko ya kumhusisha na kifo cha aliyekuwa makamu wa rais marehemu George Saitoti .
Sonko amedai kwamba kuna njama ya kumuua yeye pamoja na naibu wa rais William Ruto . Kibicho amewaambia polisi kwamba hatua ya Sonko kutoa madai hayo ni kukiri kufanya uhalifu na amesema atamshtaki Sonko kwa kumharibia jina.