Utata kuhusu kiti cha Ugavana jijini

Igathe: Kujiuzulu kwangu kama naibu gavana hakukufanywa rasmi

Kupitia wasilisho maalum kwa mahakama Igathe amesema kujiuzulu kwake hakukutambuliwa na spika wa bunge la kaunti

Muhtasari
  • Igathe alikuwa akijibu kesi ambayo mpiga kura mmoja  Patrick Kiiru amewasilisha kesi mahakamai kupinga uchaguzi mdogo Nairobi uliofaa kuandaliwa februari tarehe 18 .
  • Kiiru amesema tume ya uchaguzi nchini IEBC haina mamlaka ya kuitisha uchaguzi kuziba nafai ya gavana hasa wakati ambapo kuna naibu wa gavana anayefa kuiziba nafasi hiyo .

 

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko na Bwana Igathe

Kizungumkuti sasa  kimeibuka kuhusu siasa za kumrithi Mike Sonko katika jiji la Nairobi baada ya naibu gavana wa zamani  Plycarp Igathe kuzuka na madai kwamba hatua yake ya kujiuzulu kutoka nafasi hiyo haikuwahio kufanywa kuwa rasmi  na aaitaka mahakama kuingilia kati na kuamua Iwapo kweli kujizulu kwake kulitamatishwa kwa mujibu wa sheria .

 Akikubali kwamba alijiuzulu januari  mwaka wa 2018  Igathe amesema hatua ya kaunti kukosa  kutambua kuondoka kwake afisini inamaanisha kwamba mahakama sasa inafaa kutoa usemi wake kuhusu hatua hiyo .

 Kupitia wasilisho maalum  kwa mahakama Igathe  amesema kujiuzulu kwake hakukutambuliwa na spika wa bunge la kaunti . wasilisho hilo lilitolewa tarehe 12 januari na lilifichuliwa siku ya jumatano .

 “ Ukosefu wa kufuata sheria katika kutambua kujiuzulu kwangu  na hatua ya idara za kaunti kukosa kuchukua hatua za kufanya rasmi uamuzi wangu kuondoka  kunamaanisha sasa kwamba hatima ya uamuzi wangu ipo mikononi mwa mahakama’ amesema Igathe .

Igathe alikuwa akijibu kesi ambayo mpiga kura mmoja  Patrick Kiiru amewasilisha kesi mahakamai kupinga uchaguzi mdogo Nairobi uliofaa kuandaliwa februari tarehe 18 .

Kiiru amesema tume ya uchaguzi nchini IEBC haina mamlaka ya kuitisha uchaguzi kuziba nafai ya gavana hasa wakati ambapo kuna naibu wa gavana anayefa kuiziba nafasi hiyo .

 Uchaguzi mdogo utabadilisha mkondo wa siasa jijini kwani utamaanisha kwamba wanaoshikilia naasi hizo watafanya hivyo kwa muda mfupi . Mpiga kura huyo amesema Igathe ndiye anauefaa kuchukua usukani kama gavana wa jiji la Nairobi  .Kesi  hiyo itasikizwa jumatano na jaji Weldon Korir .