Siasa za ghasia

Mudavadi araia pawepo kuvimiliana kisiasa kabla ya uchaguzi wa 2022

Aliongeza : “ Tusiwaruhusu wanasiasa kuwafanya wakenya kuwaua wenzao au kuwajeruhi’

Muhtasari
  •  Siku inayofuata mkutano wa naibu wa rais William Ruo ulivurugwa na vijana wanaounga mkono BBI katika soko la Burma .
  • Mudavadi pia amewatahadharisha wakenya dhidi ya wanasisa wasiojishughulisha na masuala ambayo yanawaathiri wananchi na badala yake wanapiganaia maslahi yao .
Musalia Mudavadi

 Kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi ameonya kuhusu ongezeko la visa vya uhasama wa kiasia kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao .

 Mudavadi amesema  mtindo wa siasa zilizoshuhudiwa wiki iliyopita ni kumbukumbu ya ghasia zilizoonekana wakati wa uchgauzi wa 2007 na baadaye  kulifanya baadhi ya viongozi kujipata katika mahakama ya ICC .

 “ Aina hii ya siasa  tunayoona  ambapo watu wanatupa mawe….nataka kukashifu vitendo kama hivyo  .Nilikuwa katika kundi la upatanisho la Koffi Annan  tulienda ICC kwa sababu ya siasa chafu..’ amesema

Aliongeza : “ Tusiwaruhusu wanasiasa kuwafanya wakenya kuwaua wenzao au kuwajeruhi’

 Mudavadi alikuwa akizungumzia  tukio la  jumatano wiki jana wakati makundi ya vijana yalipourushia mawe msafara wa kiongozi wa ODM Raila  Odinga alipokuwa katika kituo cha magari cha Githurai .

 Siku inayofuata mkutano wa naibu wa rais William Ruo ulivurugwa na vijana wanaounga mkono BBI katika soko la Burma .

Mudavadi pia amewatahadharisha wakenya dhidi ya wanasisa wasiojishughulisha na masuala ambayo yanawaathiri wananchi na badala yake wanapiganaia maslahi yao .