Haki

Mwaname wa Kibra aliyemkojolea mtoto katika sehemu zake za siri kufungwa miaka minne jela

Hakimu amesema mtuhumiwa ana muda wa siku 14 kukata rufaa dhidi ya hukumu aliopewa .

Muhtasari
  • M.A  alihukumiwa na  hakimu mkuu Esther  Boke baada ya mwendesha mashtaka  Nancy Kerubo  kumsomea mashtaka  na ushahidi wa hatia yake .
  •  Mtuhumiwa polisi wamesema alimkojolea mtoto katika sehemu zake za siri januari tarehe 27 katika mtaa wa mabanda wa Deep Sea ,Kibra

Mwanamme mwenye umri wa miaka 56  amehukumiwa kifungo cha miaka mine jela baada ya kukiri shtaka la kumfanyia mtoto mwenye umri wa miaka 3 kitendo kisicho cha kawaida .

M.A  alihukumiwa na  hakimu mkuu Esther  Boke baada ya mwendesha mashtaka  Nancy Kerubo  kumsomea mashtaka  na ushahidi wa hatia yake .

 Mtuhumiwa polisi wamesema alimkojolea mtoto katika sehemu zake za siri januari tarehe 27 katika mtaa wa mabanda wa Deep Sea ,Kibra

Kulingana na stakabadhi ya mashtaka mtoto huyo alikuwa ameachwa na mamake kwa jirani yao na baadaye akaonekana na jirani mwingine akiingia katika nyumba ya mshukiwa  . Tukio hilo  liliripotiwa kwa majirani wengine  waliotaka kujua kilichokuwa kikifanyika  na baadaye mshukiwa alionekana kuwashambulia majirani waliotaka kujua Iwapo mtoto huyo alidhulumiwa kwa njia yoyote .

 “ Walipofkika katika mlango wa mshukiwa walimpata mtoto akiwa amebeba suruali yake ya ndani na alipohojiwa alisema mtuhumiwa alikuwa amemkojelea katika sehemu za utupu’

 Hakimu amesema mtuhumiwa ana muda wa  siku 14 kukata rufaa dhidi ya hukumu aliopewa .