Wauguzi watangaza kusitisha mgomo wao

Muhtasari

• Uamuzi huu unaambatana na agizo la   Mahakama iliwaagiza wauguzi wote  kurejea kazini mara moja.

• Mgomo huo umedumu kwa siku 79.

Katibu mkuu wa muungano wa kitaifa wa Wauguzi - KNUN Seth Panyako
Seth Panyako kutoka muungano Wauguzi Katibu mkuu wa muungano wa kitaifa wa Wauguzi - KNUN Seth Panyako

Muungano wa wauguzi nchini(KNUN) umetangaza kusitisha mgomo wao uliyokuwa umedumu kwa siku 79.

Uamuzi huu unaambatana na agizo la   Mahakama ya kusuluhisha mizozo ya leba iliwaagiza wauguzi wote wanaogoma siku ya Jumatatu kurejea kazini mara moja.

Katibu Mkuu wa muungano wa kitaifa wa wauguzi KNUN) Seth Panyako, siku ya Jumatano, aliwaamuru wanachama wote warudi kazini mara moja.

"Mgomo ulioanza Desemba 7, 2020 unasitishwa, wanachama wote waripoti kazini mara moja kabla ya kesho," Panyako alisema.

Panyako aliwahakikishia wauguzi kwamba muungano huo utaendelea kushinikiza na kujadiliana na waajiri kuhusu matakwa yao wakiwa kazini.

Muungano wa wauguzi ulikosoa hatua ya baadhi ya serikali za kaunti kuwafurusha wauguzi kutoka nyumba za za serikali. Panyako alitaja hatua hiyo kama kinyume cha sheria.

 "Hakuna muuguzi hata mmoja aliyekufa kwa COVID-19 wakati tulipokuwa tukigoma, ”alisema

Jaji wa Mahakama wa mahakama ya kushughulikia mizozo ya Leba Maureen Onyango siku ya Jumatatu aliamuru wahudumu wa afya kurejea kazini.