Huzuni yatanda, mjane wa mhariri wa KBC aahidi kulea wanawe

Muhtasari

 • "Nilikuwa namngojea aje kukagua hati hiyo na ikiwa ni sawa, aiwasilishe kwa mhadhiri ili amalize kozi yake," alisema, akiongeza kwamba alikuwa amepata pesa kumsajili Betty kwa shahada ya PhD.   

 
• "Kama vile nilikuwa nikiwa nusu yatima wakati babangu alifariki, wauaji pia wamewafanya watoto wangu wawe mayatima."

Marehemu Betty Barasa
Betty Barasa Marehemu Betty Barasa
Image: Maktaba

TAARIFA YA GORDON OSEN 

Siku ambayo mwandishi wa habari wa KBC Betty Barasa alipigwa risasi nyumbani kwake mtaani Ngong, mumewe alikuwa amechapisha tasnifu yake ya mwisho tayari kuwasilishwa kwa shahada ya uzamili.

Geoffrey Namachanja alisema mauaji ya kinyama ya mkewe wa miaka 17 mbele ya watoto wake watatu ni piga kubwa kwa familia yake.

"Nilikuwa namngojea aje kukagua hati hiyo na ikiwa ni sawa, aiwasilishe kwa mhadhiri ili amalize kozi yake," alisema, akiongeza kwamba alikuwa amepata pesa kumsajili Betty kwa shahada ya PhD.

 

"Kama vile nilikuwa nikiwa nusu yatima wakati babangu alifariki, wauaji pia wamewafanya watoto wangu wawe mayatima."

Alizungumza jana wakati wa misa ya wafu ya mhariri wa video aliyeuawa, katika makafani ya Montezuma Monalisa jijini Nairobi.

Huku akigeukia jeneza lililobeba mwili wa mkewe, Geoffrey alisema;

 "Betty mke wangu, samahani lazima uende hivi. Nitawatunza watoto na kudumisha maisha yako."

Iliibuka pia kwamba wakati Betty alikuwa akipigwa risasi, shemeji yake Edwin Namachanja — mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Maranda — alimpigia simu mumewe kumjulia hali.

Geoffrey alichukua simu, lakini kulikuwa na virumai nyuma na alisikia tu mtu akisema "huyu ndiye amepatiwa ruhusa." Kisha Geoffrey akamwambia kakake kwamba anempigia baadaye.

"Aliposema atanipigia simu baadaye, nilifikiri kwamba labda alikuwa amechelewa kufika nyumbani na hivyo kushikwa na polisi kwa sababu ya kafyu na alikuwa akijaribu kujitetea," Edwin aliambia waombolezaji wakati wa misa.

Dakika chache baadaye, binti ya Geoffrey alimpigia simu na Edwin alipochukua simu hiyo, alikuwa akilia na kutetemeka, akipiga mayowe.

 "mjomba, mjomba, mjomba mjomba"

"Nilimwambia Indiana (binti ya Betty) ampe baba yake simu," alisema.

Mwishowe Geoffrey alizungumza naye, alisema mara kwa mara: "Wamemuua mke wangu."

"Nilishtuka, nikamwambia kaka yangu awe jasiri, kwa sababu ya kuwapa nguvu watoto," Edwin alikumbuka.

"Ikiwa simu inaweza kuokoa maisha, basi simu yangu kwa kaka yangu ingeweza kuokoa shemeji yangu," Edwin alisema.

Betty alizikwa nyumbani kwake Oloolua eneo la Ngong 'katika hafla ya kibinafsi.