Mshukiwa wa 3 wa mauaji ya afisa wa tume ya ardhi afikishwa mahakamani

Muhtasari

• Jennifer aliripotiwa kutoweka baada ya mumuwe kumsindikiza ofisini mwake na baada ya sakasaka  mwili wake ulipatikana umetupwa katika msitu wa Ngong.

Jennifer Wambua
Jennifer Wambua
Image: HISANI

Mshukiwa wa mauaji ya Jennifer Wambua ambaye alikuwa afisa wa tume ya ardhi nchini (NLC), Peter Njenga kwa jina la utani Sankale anafikishwa mahakamani leo (Jumatatu).

Ndegwa mwenye umri wa miaka 44 alikuwa amewekwa korokoroni baada ya upande wa mashtaka kuomba siku 14 zaidi kuwezesha kukamilisha uchunguzi kuhusu uhusiano wake na mauji ya Jennifer.

Jennifer aliripotiwa kutoweka baada ya mumuwe kumsindikiza ofisini mwake na baada ya sakasaka  mwili wake ulipatikana umetupwa katika msitu wa Ngong.

Kulingana na ripoti ya maafisa wa DCI wanaochunguza mauji yake ni kwamba Jennifer Wambua, huenda hakutekwa nyara kabla ya kutoweka kwake.

Inaaminika kuwa alipanda matatu kuelekea Ngong, baada ya kushauriwa na mhubiri mmoja aliyemtaka kwenda kufanyiwa maombi ili apate kupona msongo wa mawazo. Polisi wamtia mbaroni mwanamume anayedaiwa kumnyonga.

Jamaa zake walipata mwili wake katika hifadhi ya maiti ya City mjini Nairobi na polisi walisema kwamba mwili wa Jennifer Wambua ulipatikana katika eneo la Ngong kabla ya kupelekwa kwa hifadhi ya maiti ya City.