USANII

Joe Mfalme awakashifu waliomcheka

Adai kuwa baadhi ya wanakijiji walimtilia shaka na kumcheka alipoamua kuwa DJ miaka 12 iliyopita. Joe amekamilisha kumjengea mamaye nyumba.

Muhtasari

•Alipochujwa redioni mwezi uliopita kwa madai ya uchochezi dhidi ya wanadada

•Awasuta waliomtilia shaka na kumcheka alipoamua kuwa DJ.

Dj-Joe-Mfalme-700x466
Dj-Joe-Mfalme-700x466

Mcheza santuri na aliyekuwa mtangazaji kwenye stesheni ya redio ya Homeboyz, DJ Joe Mfalme ameonekana mwenye bashasha baada ya kukamilisha kujengea mamake makao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Joe amewahakiki waliomtilia shaka na kumcheka miaka kumi na miwili iliyopita alipoamua kujitosa kwenye sekta ya usanii wa kucheza santuri.

“Wengi kule kijijini walinicheka na kujaribu kunikatisha tamaa huku wakiambia wazazi wangu kuwa kijana yao ameamua kuwa mkora” Joe alichapisha kwenye Instagram yake.

Amekiri kuwa kazi yake ya kucheza santuri ndiyo imemwezesha kununua shamba na kumjengea mama yake nyumba.

“Hii dunia usidharau kazi ya mtu. Nimesoma kuwa chochote unachoamua kufanya, tia bidii na uwe na nidhamu na utafanikiwa kwa neema zake Mola,” DJ huyo aliyepoteza kazi yake redioni Homeboyz baada ya madai uchochezi dhidi ya wanadada kwenye show yao kumkumba .