MASAIBU YA GAVANA WAN WAJIR

Kamati ya seneti yapendekeza kutimuliwa kwa gavana Mohamud

Kamati imempata gavana wa Wajirna kosa la utovu wa nidhamu na ukiukaji wa katiba

Muhtasari

•Mohamud aling'atuliwa tarehe ishirin9i na saba Aprili

•Maseneta 24 wanahitajika kudhibisha kung'atuliwa kwa gavana

Gavana Mohamud
Gavana Mohamud
Image: HISANI; the star

Kamati ya maseneta kumi na mmoja limependeza kung’atuliwa mamlakani kwa gavana wa Wajir Mohammed Abdi Mohamud.

 Hii ni baada ya kamati hiyo kumpata gavana Abdi na hatia ya ukiukaji wa vipengele vya katiba vya manunuzi na ugavi wa rasilimali ya kaunti na usimamizi wa pesa za uma.

Kamati hiyo iliyoongozwa na seneta wa Nyamira, Okong’o Omogeni  hata hivyo imedai kuwa wajumbe wa kaunti ya Wajir walikosa kudhibitisha kosa la matumizi mabaya ya ofisi na utovu wa nidhamu. Gavana Abdi alikuwa amekisiwa kumruhusu bibi yake kuchukulia baadhi ya shughuli za serikali ya kaunti.

Wajumbe wa kaunti ya Wajir walikuwa wamemshtaki gavana kwa kosa la matumizi mabaya ya pesa za utunzi wa mifumo ya afya, utovu wa nidhamu na ukiukaji wa katiba. 37 kati yao walipiga kura kumg’atua huku 10 wakipinga mwishoni wa mwezi wa Aprili.

Kamati hiyo ilikutana siku ya Jumatano na Alhamisi na kisha wikendi wakaandika ripoti waliyowasilisha leo Okong’o. Maseneta wote wanatarajiwa kupiga kura baadae leo ili kuamua ikiwa Gavana Abdi atang’atuliwa.  Angalau maseneta 24 kati ya 47 waliochaguliwa wanahitajika kudhibitisha pendekezo hilo.