HONGERA ATWOLI

Atwoli avunja rekodi kwa kuchaguliwa kama mwanachama wa ILO kwa mara ya nne mfululizo

Atwoli ataendelea kuwakilisha wafanyakazi wote barani Afrika kwenye shirika la ILO kwa kipindi cha miaka minne (2021-2024)

Muhtasari

•Katibu wa COTU alivunja rekodi ya kuwa mwanachama wa kwanza kuchaguliwa kwa mara nne mfululizo

•Atwoli ambaye ni  baadhi ya wagombeaji waliopata kura nyingi zaidi atakuwa na jukumu la kutetea wafanyakazi wa bara Afrika kwa kipindi cha miaka minne (2021-2024)

Katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli
Katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli

Katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli amevunjam rekodi kwa kuchaguliwa tena kwa mara ya nne kama mwanachama wa shirika la kazi la kimataifa (ILO) lililoko jijini Geneva, Uswisi.

Atwoli alichaguliwa kuendelea kuwakilisha bara Afrika kwenye shirika hilo kwenye kipindi cha kongamano la kimataifa la kazi asubuhi ya siku ya Jumatatu.

Kupitia ujumbe kwa wanahabari, naibu katibu mkuu wa COT, Benson Okwaro  amesema kuwa ushindi huo umemfanya mwanachama wa kwanza kuchaguliwa kwa mara nne mfululizo .

Hii ni ishara kubwa kuwa viongozi wa miungano ya wafanyakazi barani Afrika wana imani kubwa na uongozi wa Bw Atwoli” Okwaro alisema.

ILO ni shirika la Umoja wa Mataifa ambalo ambalo lilianzishwa mwaka wa 1919 na linaangazia kukuza haki za kijamii na haki za wafanyakazi.

Atwoli ambaye ni  baadhi ya wagombeaji waliopata kura nyingi zaidi atakuwa na jukumu la kutetea wafanyakazi wa bara Afrika kwa kipindi cha miaka minne (2021-2024)

Muungano wa COTU umejivunia ushindi huo huku ukisifia uongozi wa Atwoli.

Kama COTU tunajivunia sana kuhusishwa na Dr Atwoli na kwa uongozi wake, ushauri  na mwongozo wake. Kwa kweli, Atwoli anapongezwa kimataifa kufuatia uongozi wake imara na kujitolea  kutetea wafanyakazi  kote ulimwenguni” Muungano wa COTU ulisema.

Mwezi wa Aprili, Atwoli alichaguliwa kama Katibu Mkuu wa COTU  kwa mara ya tano bila kupingwa. Amekuwa akiongoza muungano huo tangu mwaka wa 2001.