Watahiniwa wa KCPE 2020 kujua shule za upili watakazojiunga nazo leo

Wale ambao hawataridhishwa na shule ambazo watoto wao watakuwa wameitwa watapewa fursa ya kuomba uhamisho kupitia mtandao wa tovuti ya wizara ya elimu kabla ya kufunguliwa kwa shule.

Muhtasari

•Mwezi wa Mei, waziri wa elimu Prof George Magoha alitangaza kuwa kila mmoja wa walio kalia mtihani wa KCPE 2020 atapata nafasi katika shule ya sekondari

CS magoha
CS magoha

Watahiniwa wa mtihani wa KCPE 2020 wanatarijiwa kujua shule za upili ambazo watakuwa wanajiunga nazo siku ya Jumanne.

Baada ya kupokea wito wa shule, wanafunzi hao wanatarajiwa  kujiunga na shule za upili tarehe 2 mwezi  wa Agosti.

Wazazi ambao hawataridhishwa na shule ambazo watoto wao watakuwa wameitwa watapewa fursa ya kuomba uhamisho kupitia mtandao wa tovuti  ya wizara ya  elimu kabla ya kufunguliwa kwa shule.

Kuchaguliwa kwa watahiniwa wa KCPE 2020 kulifanyika mwezi Juni baada ya kuchelewesha kwa muda.

Mwenyekiti wa muungano wa wazazi, Nicholas Maiyo alikosoa hatua ya serikali kupatia wazazi muda kidogo kati ya kuchaguliwa kwa wanafunzi kwenye shule za upili na wakati wa kuijunga na shule zile.

Mwezi wa Mei, waziri wa elimu Prof George Magoha alitangaza kuwa kila mmoja wa walio kalia mtihani wa KCPE 2020 atapata nafasi katika shule ya sekondari

“Tunadhamiria kufanya kazi na mashirika husika kuhakikisha kuwa hakuna mtahiniwa atakoa nafasi katika shule ya Sekondari” Magoha alisema.

Watahiniwa zaidi ya milioni moja walikalia mtihani wa KCSE uliofanyika mwezi wa Machi mwakani  huku 8,091 wakiandikisha alama 400 kwenda juu. 8091 hao pamoja na wanafunzi tano bora kwa kila kaunti watapata nafasi kwenye shule za kitaifa.

Watahiniwa ambao 243,320 waliweza kuzoa kati ya alama 301 na alama 400 wataweza kujiunga na shule za kaunti na za extra-county.

Idadi kubwa zaidi  ya wanafunzi inatarajiwa kuchaguliwa kujiunga na shule za kutwa