Polisi wawinda majambazi waliopokonya maafisa bunduki na kuvamia benki Machakos

Pale ndani ya benki waliamurisha wafanyakazi na wateja kulala chini kabla ya kufanya shughuli zao na kutoka.

Muhtasari

•Kulingana  na mashahidi, genge la majambazi watatu lilishambulia polisi wawili waliokuwa wameshika doria katika benki hilo, wakawapokonya bunduki zao na kuingia ndani ya benki

•Uvamizi huo unasemekana kuchukua muda wa dakika 10 kabla ya majambazi hao kuweza  kutoroka kwa gari licha ya kukimbizwa na polisi.

crime scene 1
crime scene 1

Habari na Cyrus Ombati

Polisi upande wa Machakos wanawinda genge la majambazi walioiba bunduki za polisi na kuvamia benki ya Equity katika mji wa Matuu.

Kulingana  na mashahidi, genge la majambazi watatu lilishambulia polisi wawili waliokuwa wameshika doria katika benki hilo, wakawapokonya bunduki zao na kuingia ndani ya benki.

Pale ndani ya benki waliamurisha wafanyakazi na wateja kulala chini kabla ya kufanya shughuli zao na kutoka.

Polisi walidai kuwa majambazi hao pia walishambulia maafisa waliofika kwenye eneo la tukio kwa risasi na wanashuku kuwa mmoja wao alijeruhiwa kwenye harakati hiyo.

Uvamizi huo unasemekana kuchukua muda wa dakika 10 kabla ya majambazi hao kuweza  kutoroka kwa gari licha ya kukimbizwa na polisi.

Polisi waliendelea  kuwafuata majambazi hao kwenye barabara kuu ya kuelekea Nairobi huku vizuizi vya barabara vikiwekwa kwenye maeneo mbalimbali.

Inadaiwa kuwa baada ya hatua kadhaa genge hilo lilibadilisha chombo chao cha usafiri na kuchukua pikipiki