COVID 19: Wagonjwa 1950 waendelea kupokea matibabu, Vifo 6 zaidi vyaripotiwa

Kufikia sasa serikali ya Kenya imeweza kupeana chanjo 4, 902, 772.

Muhtasari

•Kiwango cha maambukizi nchini kwa sasa ni 2.5   huku jumla ya visa ambavyo vimewahi kuripotiwa ikifikia 252, 628.

•Kufikia jana watu 1,414, 202 walikuwa wamechajwa kikamilifu huku wengine 3, 493, 570 wakiwa wamepokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya Corona.

Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MAKTABA

Wizara ya afya hivi leo imeripoti visa vipya 129 vya waathiriwa wa COVID 19 kutoka kwa sampuli ya watu 5110 waliopimwa katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita.

Kiwango cha maambukizi nchini kwa sasa ni 2.5   huku jumla ya visa ambavyo vimewahi kuripotiwa ikifikia 252, 628.

Raia 12 wa kigeni ni miongoni mwa 129 waliopatikana na virusi hivyo nchini.

Kaunti ya Nairobi iliripoti visa vingi zaidi leo (20) ikifuatwa na Trans Nzoia ambayo imeripoti visa 16, Nakuru 13, Turkana 10 huku kaunti zingine zikiandikisha visa chini ya 10.

Wagonjwa 209 wameweza kupata afueni ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita, na kufikisha idadi ya waliowahi kupona nchini hadi 246, 027.

Jumla ya walioangamia kutokana na maradhi hayo sasa imefikia 5, 255 baada ya vifo 6  zaidi kuripotiwa.

Kwa sasa wagonjwa 521 wamelazwa hospitalini  huku wengine 1429 wakiendelea kuhudumiwa nyumbani. Wagonjwa 32 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Chanjo ya Corona

Kufikia jana watu 1,414, 202 walikuwa wamechajwa kikamilifu huku wengine 3, 493, 570 wakiwa wamepokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya Corona.

Kufikia sasa serikali ya Kenya imeweza kupeana chanjo 4, 902, 772.