Polisi wachunguza mauaji ya mwanahabari wa BBC Nairobi

Muhtasari

•Uchunguzi wa awali unaashiria bi Kate Mitchell alinyongwa na mwanaume ambaye walionekana pamoja katika hoteli hiyo iliyo katika maeneo ya Kileleshwa.

•Wasimamizi walisema Mitchell alibonyeza kengele wakati vita vilikithiri ila kwa bahati mbaya akanyongwa kabla ya kupata usaidizi.

•Wapelelezi walipochungulia chini kupitia dirisha waliona mwili wa mwanaume ukiwa umelala chini ya jengo la hoteli hiyo. 

crime scene 1
crime scene 1

Polisi wanachunguza kifo cha mwandishi wa habari wa BBC ambaye mwili wake ulipatikana katika chumba chake hotelini moja jijini Nairobi

Uchunguzi wa awali unaashiria bi Kate Mitchell alinyongwa na mwanaume ambaye walionekana pamoja katika hoteli hiyo iliyo katika maeneo ya Kileleshwa.

Mwanaume anayetuhumiwa kutekeleza mauaji hayo aliaga kutokana na majeraha baada ya kuruka kutoka kwa ghorofa ya nane katika juhudi za kukimbia eneo la tukio.

Wawili hao wanadaiwa kushiriki mabishano makali kabla ya vita iliyopelekea maafa hayo kutokea.

Wasimamizi walisema Mitchell alibonyeza kengele wakati vita vilikithiri ila kwa bahati mbaya akanyongwa kabla ya kupata usaidizi.

Kamanda wa polisi jijini Nairobi Augustine Nthumbi alisema mlango wa chumba cha Mitchell ulikuwa umefungwa upande wa ndani wakati wapelelezi waliwasili.

Wapelelezi walipata mwili wa Mitchell ukiwa umelala chini huku kukiwa na vipande vya glasi zilizovunjika sakafuni.

Wapelelezi walipochungulia chini kupitia dirisha waliona mwili wa mwanaume ukiwa umelala chini ya jengo la hoteli hiyo. Baadae walibaini kuwa ulikuwa wa mawanaume ambaye alikuwa ameonekana na Mitchell hapo awali.

"Mshukiwa aliruka kutoka gorofa ya nane ya hoteli hiyo kupitia dirisha la chumba hicho baada ya kuhisi kwamba huenda walinzi wa hoteli hiyo wangempata,” Nthumbi alisema.

Bado haijabainika kilichosababisha mauaji hayo.

Mwili wa marehemu  ulipelekwa katika mochari huku uchunguzi wa mwili ukiwa umesubiriwa.

Mwanahabari huyo ambaye ambaye aliwasili nchini siku chache zilizopita alikuwa anafanya kazi katika ofisi za BBC nchini Ethiopia.

Kwa kawaida ofisi hizo za Addis Ababa husimulia hadithi za kweli kuhusu uhamiaji usio salama na haramu, afya na maendeleo ya vyombo vya habari.

(Utafsiri: Samuel Maina)