Jamaa atiwa mbaroni kwa kutosheleza kiu chake cha tendo la ndoa na ndama wa shemejiye Kericho

Muhtasari

•Langat alipokuwa kitandani alimsikia ndama wake akilia kwa maumivu akatoka polepole ili  kuangalia kilichokuwa kimemshambulia.

•Langat aliposonga karibu zaidi aligundua kwamba ni shemeji yake Lamar ambaye alikuwa uchi wa mnyama baada ya kumaliza kufanya kitendo hicho cha aibu na kuchukiza.

Pingu
Image: Radio Jambo

Hali ya mshtuko ilitanda katika kijiji cha Kamanamsim, eneo la Iten, kaunti ya Kericho asubuhi ya Jumapili baada ya jamaa mmoja kupatikana akitosheleza hamu yake ya ngono na ndama.

DCI wameripoti kwamba Kennedy Lamar 31, alikamatwa baada ya mwenye ndama Fancy Langat kumpata katika kitendo kile na kupiga nduru kubwa iliyovutia wanakijiji.

Langat alipokuwa kitandani alimsikia ndama wake akilia kwa maumivu akatoka polepole ili  kuangalia kilichokuwa kimemshambulia.

Alipokaribia zizi la ng'ombe aliona kivuli cha mwanaume kwenye giza ambacho kilikuwa kinasonga kando na ndama wake.

Langat aliposonga karibu zaidi aligundua kwamba ni shemeji yake Lamar ambaye alikuwa uchi wa mnyama baada ya kumaliza kufanya kitendo hicho cha aibu na kuchukiza.

Kuona hayo alipiga uyowe mkali na kuwaita majirani ambao waliachwa vinywa wazi kuona yaliyokuwa yametendeka pale.

Chifu wa eneo hilo aliongoza wanakijiji kumkamata mshukiwa na wakampeleka hadi kituo cha polisi cha Litein ambako anazuiliwa akisubiri kufikishwa mahakamani.