Muhtasari
•Watatu hao walikuwa wanaelekea nyumbani baada ya kunyolewa walipoamua kuogelea kidogo.
Biwi la simanzi limetanda katika eneo la Gatanga, kaunti ya Murang'a baada ya wavulana watatu kufa maji walipokuwa wanaogelea mtoni Kiama siku ya Jumapili.
Watatu hao walikuwa wanaelekea nyumbani baada ya kunyolewa nywele katika kinyozi kimoja mtaani Kirwara walipoamua kuogelea kidogo.
Wapiga mbizi kutoka eneo hilo waliweza kutoa miili ya wavulana wawili jioni ya Jumapili huku mwili mmoja uliosalia ukitolewa Jumatatu asubuhi.
Wavulana hao walikuwa wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi ya Mabae iliyo eneo la Gatanga.