AY amwandikia mkewe ujumbe maluum kwa kupata mtoto wa pili

Muhtasari

•AY amwandikia mkewe Mabel ujumbe maalum kwa kuweza kupata mtoto wao wa pili

•Hakuna anayejua hadithi  yetu katika miaka 13 iliyopita kama sio  sisi, Lakini nataka hasa kukushukuru kwa kila kitu. 

AY COMEDIAN
AY COMEDIAN
Image: Hisani

Mcheshi maarufu kutoka Nigeria Richard Ayodeji almaarufu AY amwandikia mkewe Mabel ujumbe maalum kwa kupata mtoto wao wa pili.

Mabel alipata mtoto wa pili wiki jana ambapo mumewe AY hakuficha furaha yake baada ya kupata habari hizo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram AY alishukuru mama wa watoto wake na kumtaja kuwa mvumilivu kwenye ndoa licha ya changamoto si haba zilizoyumbisha ndoa yao.

"Hakuna anayejua hadithi  yetu katika miaka 13 iliyopita kama sio  sisi. Lakini nataka hasa kukushukuru kwa kila kitu. Asante kwa kuwapuuza wambea wote. Asante kwa kuchukua muda kutoka kwa kazi zako nyingi za ndani na nje ya nchi ili kujiandaa kwa ajili ya Ayomide,"alisema AY.

Isitoshe alimpongeza mkewe kwa uvumilivu aliokuwa nao hasa kwenye kipindi hicho cha miezi tisa.

"Nakushukuru kwa muda wa miezi tisa kwa kubeba ujauzito usiopendeza na usio na raha, kupoteza hamu ya kula chakula ulichokifurahia hapo awali, kutoweza kunywa glasi ya divai uipendayo, na bila shaka yale yote ya kustaajabisha. maumivu ambayo huja muda mrefu kabla ya leba kuanza."