Youtube, Twitter na Facebook zazima huduma zao nchini Urusi

Muhtasari

• Kampuni za Facebook na YouTube Zimezuia vyombo vya habari vya serikali ya Urusi kusambaza matangazo na kunufaika na mapato kwenye mitandao hio kupitia video zao.]

• Hatua hizi zinajiri baada ya kuwa na shinikizo kubwa la kampuni kubwa za mitandao ya kijamii kuchukua hatua dhidi ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine pamoja na kuzuia taarifa za propaganda kutoka Urusi.

Kampuni za Facebook na YouTube Zimezuia vyombo vya habari vya serikali ya Urusi kusambaza matangazo na kunufaika na mapato kwenye mitandao hio kupitia video zao.

Kwa upande wake, Twitter pia imesimamisha matangazo yote yanayotoka nchini Urusi na Ukraine katika harakati zinazolenga kuzuia usambazaji wa taarifa zitakazochochea vita kati ya Ukraine na Urusi.

Hatua hizi zinajiri baada ya kuwa na shinikizo kubwa la kampuni kubwa za mitandao ya kijamii kuchukua hatua dhidi ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine pamoja na kuzuia taarifa za propaganda kutoka Urusi.

Wiki hii Senator wa jimbo la Virginia, nchini Marekani aliandika barua kwa kampuni zote za mitandao ya kijamii kama Meta, Twitter, Google, Alphabet, TikTok, Reddit na Telegram kuwaomba waongeze ulinzi dhidi ya taarifa zinazotoka Urusi.