Uhuru amuomboleza Kibaki kama rais shupavu na mwanauchumi bora Afrika

Muhtasari

• Rais alisema kuwa Kibaki alikuwa mwanauchumi aliyethibitishwa ambaye tajriba na uwezo wake wa kubadilisha uchumi ulitambuliwa sio tu nchini bali kimataifa.

 

Rais Uhuru Kenyatta na mama wa taifa Margaret Kenyatta wakiajiandaa kuelekea uwanja wa Nyayo kwa misa ya wafu ya hayati rais mutastaafu Mwai Kibaki
Rais Uhuru Kenyatta na mama wa taifa Margaret Kenyatta wakiajiandaa kuelekea uwanja wa Nyayo kwa misa ya wafu ya hayati rais mutastaafu Mwai Kibaki
Image: PSCU

Rais Uhuru Kenyatta alimpongeza mtangulizi wake marehemu Rais Mwai Kibaki wakati wa ibada ya wafu siku ya Ijumaa.

Uhuru alimtaja Kibaki kama kiongozi mahiri, muungwana aliyetukuka na mwanasiasa mwenye kanuni na maono ambaye alisimamia ukuaji wa uchumi wa nchi na kuweka msingi wa ukuaji wa siku zijazo.

"Kibaki alikuwa wa kuigwa na hakuamini kwa majigambo,"Uhuru alisema katika hafla hiyo iliyofanyika katika uwanja wa Nyayo.

Rais alisema kuwa Kibaki alikuwa mwanauchumi aliyethibitishwa ambaye tajriba na uwezo wake wa kubadilisha uchumi ulitambuliwa sio tu nchini bali kimataifa.

Alisema uongozi wa maono wa rais Kibaki ulitoa dira ya 2013 inayoipa nchi njia ya maendeleo makubwa.

"Ingawa Kibaki amepumzika, huduma yake kwa nchi yetu haitatulia hadi awamu ya mwisho ya maono yake kwa nchi yetu yakamilike," Rais alisema.

Rais, ambaye aliongoza angalau marais watatu na wawakilishi wa nchi mbalimbali katika kutoa heshima ya mwisho kwa Kibaki, alisema marehemu rais alikuwa mmoja wa wasomi bora zaidi wa kiuchumi Afrika kuwahi kuwa nao.

Rais Kenyatta alisema kuwa rais huyo wa zamani wa nchi alikuwa mtu mwenye bidii na mwenye kusamehe ambaye alishughulikia changamoto zake kwa uangalifu na mbali na mwanga wa umma.

Alitaja tukio la baada ya uchaguzi wa 2007 ambapo yeye na kiongozi wa Upinzani Raila Odinga walijadiliana kumaliza umwagakaji wa damu na kukubaliana kugawana serikali kwa misingi ya nusu kwa nusu.