Maandamano ya Azimio kufanyika kila Jumatatu na Alhamisi - Raila atangaza

Raila alikuwa ametangaza kuwa maandamano ya upinzani yangefanyika Jumatatu kila wiki.

Muhtasari

• "Tumeanza vita. Kila Jumatatu kutakuwa na mgomo. Kutakuwa na maandamano. Vita imeanza haitaisha mpaka wakenya wapate haki yao," Raila alisema.

Image: Facebook

Kinara wa upinzani Raila Odinga ametangaza kuwa Muungano wa Azimio La Umoja One Kenya utaendesha maandamano ya kupinga utawala wa rais William Ruto mara mbili kwa wiki.

Akihutubia wanahabari siku ya Jumanne, Raila alitangaza kuwa watakuwa wakiingia barabarani kila Jumatatu na Alhamisi kila wiki.

Kivumbi kitaanza wiki ijayo.

“Katika awamu ya pili tutaanza maandamano Jumatatu na Alhamisi kuanzia wiki ijayo,” alisema.

Mnamo Jumatatu, Raila alikuwa ametangaza kuwa maandamano ya upinzani yangefanyika Jumatatu kila wiki.

Akizungumza katika eneo la Kamukunji Raila alisema maandamano ya kushinikiza serikali yalikuwa yaendelea kuafanyika kila siku ya Jumatatu hadi pale serikali ingetekeleza matakwa ya upinzani na wananchi.

"Tumeanza vita. Kila Jumatatu kutakuwa na mgomo. Kutakuwa na maandamano. Vita imeanza haitaisha mpaka wakenya wapate haki yao," Raila alisema.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO.