LIGI YA LALIGA

Hongera Atletico!!- Mabingwa wa Laliga 2020/2021

Atletico Madrid imeshinda kombe la Laliga na pointi 86 ikifuatwa kwa karibu na Real Madrid, 84, na Barcelona ,79.

Muhtasari

•Atletico Madrid imeshinda kombe la Laliga na pointi 86 ikifuatwa kwa karibu na Real Madrid, 84, na Barcelona ,79.

Wachezaji na na kocha wa Atletico washerehekea
Wachezaji na na kocha wa Atletico washerehekea
Image: HISANI

Klabu ya Atletico Madrid imeibuka mshindi wa kombe la Uhispania almaarufu kama Laliga.

Atletico ilishinda kombe hilo siku ya Jumamosi baada ya kucharaza Real Valladoid mabao mawili kwa moja na kujihakikishia nafasi hiyo ya kileleni. Mabao ya Atletico yalifungwa na Correa na Luiz Suarez huku Oscar Plano akifungia Valladoid.

Klabu hiyo inayoongozwa na Diego Simeone iliweza kuzoa alama 86 msimu huu huku ikifuatwa nyuma kwa karibu na mahasidi wa jadi Real Madrid na Barcelona zikijizolea alama 84 na 79 mtawalia.

Hii ni mara ya 11 klabu hiyo kushinda kombe la Laliga huku ikishinda mara ya mwisho msimu wa 2013/2014.