Wajir Women Rep Fatuma Gedi: Baada ya video ya ngono kusambaa, nyota yangu ilianza kung’ara

Muhtasari

• Mbunge wa kaunti ya Wajir Fatuma Gedi alisema mkanda wa video ya ngono iliyorubuniwa kuwa yeye ulimfungulia nyota yake katika siasa.

Image: Ezekiel Aming'a

Mwakilishi wa kike katika kaunti ya Wajir, Fatuma Gedi sasa anadai kwamba mkanda wa video ya ngono ambao ni bandia uliotumbuliwa mwaka 2019 ukimhusisha kama mhusika katika kitendo kile ulimfungulia baraka na bahati nyingi katika tasnia ya siasa nchini.

Katika mkanda huo uliosambazwa pakubwa na kwa mara nyingine kuwaunganisha pamoja wakenya zaidi ya milioni 10 mwaka wa 2019 ulionesha mtu ambaye alikuwa akijidai kuwa ni yeye akiwa katika kitendo hicho cha aibu.

Gedi alijitokeza wazi na kupinga kabisa kadai hayoi na kusisitiza kwamba video ile iliundwa tu na baadhi ya mahasimu wake wa kisiasa ili kuzima ndoto yake na kukana vikali kwamba mwanamke aliyeonekana pale si yeye.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee katika runinga moja nchini, Gedi alisema kwamba mkanda ule japo ulimuuma wakati watu walisema ni yeye, ulimfungulia baraka nyingi katika siasa.

“Wanaume wengine walikaa chini na kulipa pesa nyingi kutengeneza hiyo video ili waniangushe...Kuna Mungu aliye juu alikataa kuniangusha. Badala yake, baada ya video hiyo, nyota yangu ilianza kupanda na kung’ara,” alisema Gedi.

Licha ya kuvaia Ngozi ya chuma katika uso wa umma, mbunge huyo wa kaunti alisema nyuma ya pazia kitendo kile kilimuuma sana mpaka karibu kumsababishia unyongovu kutokana na kumchafulia picha yake katika uso wa umma ulimwengu mzima.

“Imenigharimu sana. Sio kitu ambacho unatamani kwa mwanamke yeyote. Kila ninapozungumza kuhusu video hiyo mimi hupata hisia chungu sana," aliongeza Gedi.

Wiki jana, mbunge huyo wa Wajir aligonga vichwa vya habari baada ya kufikisha bungeni mswada na Ushahidi aliokuwa anadai ni wa kuonesha kwamab naibu rais William Ruto ni mnyakuzi wa mashamba ya umma, katika kikao cha bunge ambacho kilibuma baada ya mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino kutamka maneno yaliyomkasirisha spika Justine Muturi na kumtaka atoke nje na alipokataa kikao kikairishwa.