Mihogo, Samaki, Biblia: Baadhi ya zawadi Ruto aliwahi kupokezwa na wafuasi wake

Ruto alianza kampeni zake mapema mwaka 2018 baada ya Handshake.

Muhtasari

• Katika kampeni zake nchini, alitembelea maeneo mbali mbali alikozawidiwa zawadi za kipekee na wafuasi wake.

Naibu rais William Ruto akipokezwa mhogo
Naibu rais William Ruto akipokezwa mhogo
Image: Facebook//WilliamRuto

Msimu wa kampeni, wanasiasa mbalimbali wanazidi kutangamana na wananchi wapiga kura, huku wakijionesha kwa ukaribu mno na wananchi kama njia moja ya kuwarai kuwapigia kura.

Katika kutangamana huko, wanasiasa wamejipata wakiombwa vitu mbalimbali na wananchi huku pia baadhi ya wananchi wapiga kura wakiwazawidi wanasiasa vitu ainati.

Kwa kawaida, imezoeleka kwamba mwananchi akiamua kumzawidi mwanasiasa basi lazima zawadi hiyo iwe yenye dhamani iliyotukuka.  Wanasiasa wengine wanazawadiwa magari ya kifahari tena mengi, wengine fedha, wengine hata helikopita za kuwasaidia kurahisisha mizunguko ya kampeni zao.

Naibu rais William Ruto
Naibu rais William Ruto
Image: Facebook//WilliamSamoeiRuto

Leo tunaangazia zawadi za ajabu ambazo mpeperusha bendera wa Kenya Kwanza, William Ruto amekuwa akipokezwa katika kampeni zake sehemu mbali mbali nchini.

William Ruto alianza kampeni zake mapema mno mnamo mwaka 2018 pindi tu rais Kenyatta walipozika tofauti zao na Raila Odinga na kuamua kufanya kazi pamoja, jamboa Ruto aliliona kama ni kusalitiwa na rais na hivyo kujitenga na mchakato huo wa Handshake.

Katika kampeni zake nchini, alitembelea maeneo mbali mbali alikozawidiwa zawadi za kipekee na wafuasi wake.

Gari la magurudumu 12

Gari la magurudumu sita la Ruto
Gari la magurudumu sita la Ruto
Image: TheStar

Mapema mwezi jana, Ruto alisimamisha mitandao ya kijamii baada ya kupakia gari la kifahari aina ya Hennessey 6x6 Veoci Raptor lililokuwa limepambwa kwa nembo za chama cha UDA pamoja na picha zake. Ruto alisema kwamba gari hilo alizawadiwa na wafuasi wake ili kufanya kampeni. Gari hilo linakisiwa kuwa la thamani ya takriban shilingi milioni 44 pesa za Kenya.

Biblia

Mnamo mwezi Machi mwaka jana, Ruto katika kampeni zake kwenye kaunti ya Nandi maeneo ya Mosoriot alipokezwa zawadi ya biblia kutoka kwa mfuasi wake mmoja. Katika picha alizopakia kwenye ukurasa wake wa Facebook, Ruto alisema kwamba ataitumia picha hiyo kuwapiga vita matapeli wa kisiasa.

Mihogo

Mwaka 2020, mkulima mmoja kwa jina Kamunyu Wambugu na mkewe walimtembelea naibu rais William Ruto katika makaazi yake rasmi eneo la Karen ambapo pamoja nao walibeba mihogo kama zawadi kwa Ruto.

Samaki

Mwaka 2018 akiwa katika ziara ya kampeni zake Nyanza, Ruto alishangazwa na kitendo cha mwanamke kwa jina Janet Ondigo aliyempokeza zawadi ya Samaki wawili huko Muhuru Bay kaunti ya Migori.