Pigo tena kwa Azimio baada ya Maaga kujiunga na Kenya kwanza

Kuondoka kwa Maaga yanafuatia kuondoka kwa Mike Sonko na mbunge mwenzake wa Kisauni Ali Mbogo

Muhtasari

•Maaga hata aliendelea kueleza kuwa Ongeri tayari alikuwa akipoteza kinyang'anyiro hicho kwani kampeni zake hazikuwa ya kushawishi wafuasi.

•Akizungumza na wanahabari, Maaga aliwaambia wanahabari kwamba uamuzi wake ulisukumwa sana  na wazee wa Bamachoge ambao walimshauri kuhamia Kenya kwanza.

Eng Josiah Maaga akiwahutubia wanahabari na wazee Jumatano Agosti 3, 2022.
Eng Josiah Maaga akiwahutubia wanahabari na wazee Jumatano Agosti 3, 2022.
Image: STAR

Josiah Maaga ambaye alikuwa mgombea mwenza wa Sam Ongeri katika kinyang'anyiro cha ugavana wa Kisii kwa tiketi ya chama cha DAP-K amewaacha Ongeri na Azimio na  kujiunga na Kenya Kwanza.

Akizungumza na wanahabari, Maaga aliwaambia wanahabari kwamba uamuzi wake ulisukumwa sana  na wazee wa Bamachoge ambao walimshauri kuhamia Kenya kwanza.

"Sina uwezo wa kufanya uamuzi kama huo peke yangu, bado ningekuwa tu naibu wa Ongeri kwa  jamii ile ile iliyonishauru kubadilisha kambi," Maaga alisema.

Maaga hata aliendelea kueleza kuwa Ongeri tayari alikuwa akipoteza kinyang'anyiro hicho kwani kampeni zake hazikuwa ya kushawishi wafuasi.

"Kampeni yake kwa kiasi kikubwa imekuwa duni na haina  ile nguvu ya kuwarai wapiga kura kumuunga mkono,'' Maaga alisema.

''Tayari tulikuwa tunapoteza ndiyo maana nakakubali uamuzi huu wa kujiondoa  kwake ili tumuunge mkono Machogu,” Aliendelea.

Hatua ya kuaga timu ya Azimio ilikuja wakati Sam Ongeri alipokuwa katika mkutano na Rais Uhuru Kenyatta katika  jimbo la Kisii.

Maaga alitangaza kuwa atamuunga mkono mgombeaji wa UDA Ezekiel Machogu kukuwa ugavana wa Kisii na William Ruto kukuwa rais.

Kuondoka kwa Maaga yanafuatia  kuondoka kwa Mike Sonko na mbunge mwenzake wa Kisauni Ali Mbogo siku chache zilizopita.

Sonko alisema kuwa UDA ilitoa ahadi za kuridhisha huku ikimtaka kuunga mkono mgombeaji ugavana wa Mombasa Hassan Omar saa chache baada ya kuachana na chama cha muungano cha Azimio la Umoja One Kenya.