Video - Raila asakata 'Jerusalema challenge'

Muhtasari

•Raila acheza Jerusalem Challenge na kufurahisha wengi

Raila Odinga

Jerusalema ni wimbo ambao umetamba pembe zote za dunia huku kila mmoja na makundi mbali mbali ya watu wakijaribu kuucheza. 

Si mmoja au wawili bali kampuni, viongozi na hata makanisani watu wamekuwa wakinengua maungo wakicheza wimbo huo katika kile wameita 'Jerusalema challenge'.

Kupitia kwenye mtandao wa twitter Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga ameweka video akiwa na kikosi cha timu ya Gor Mahia na mashabiki wengine wakifanya  'Jerusalema challenge'.  

 

Baada ya kuposti video hiyo aliandika ujumbe mfupi unaosoma,

"Nani kama baba..katika hafla ya Gor Mahia alasiri hii nilijiachilia na kutingisha mguu na timu ." Aliandika Raila.

Hizi hapa baadhi ya hisia za wakenya kuhusu video hiyo;

Robaa: Ile mguu yetu ilipona kwani ama unataka alafu utusumbue na paybill tena

Francis Jumba: Anything for you, hata kama ni madhogodhania na miguu yote ni left you're still Baba.

Amollo simba: if Baba says his dance is the new Jerusalema dance, who are we to question?

Kamu D: I like how baba dances

Hon Silas Njura E.G.H: Vivaaaaaa baba nani anakupinga

Macline Ogweno: Hongera kwa kujiunga tena na mashabiki wa Gor Mahia 

(Mhariri Davis Ojiambo)