SARAKASI ZA EMBARAMBAMBA

Je, huenda Embarambamba amewacha sarakasi?

Mwanamuziki huyo amewachilia kibao kipya ambacho hakina sarakasi zozote kama ilivyo kawaida yake.

Muhtasari

•Embarambamba ametoa wimbo unaoitwa 'Jesus is the final'

•Ana mtindo tatanishi wa kukatika kwenye nyimbo zake

CHRIS EMBARAMBAMBA
CHRIS EMBARAMBAMBA
Image: HISANI: YOUTUBE

Mwanamuziki ambaye ana mtindo tatanishi wa kukatika kwenye nyimbo zake, Christopher Nyangwara Mosioma almarufu kama Embarambamba ameachilia kibao  kipya ambacho hakina sarakasi mingi kwenye video kinyume na ilivyo kawaida yake.

The best gospel artist from kisii kenya people love nowadays Support talent support msanii embarambamba 🔊💜♥0726204282 This song tells you that in whatever you want to do in this life Without Jesus Christ you won`t succeed. This video is sponsored by The incoming Kisii County Senator Hon.Okengo Nyambane Directed By Neskon Onfleek @Tamra Creatives Agency

Katika wimbo unaoitwa 'Jesus is the final' (Yesu ndiye mwisho) ambao uliweka kwenye mtandao wa Youtube siku ya Jumatatu, Embarambamba anaonekana ametulia huku akiwa amevalia mavazi yaliyopambwa na kuzungukwa na mandhari ya kifahari.

Kwenye video hio, msanii huyo tokea upande wa Nyamira anajiwasilisha kama tajiri aliyefanikiwa maishani. Jambo hilo limeleta hisia mbalimbali miongoni mwa mashabiki waliomzoea kuwa na sarakasi mingi kwenye wimbo zake. Hizi baadhi ya hisia walizoandika mashabiki kuhusiana na wimbo ule.

Embarambamba amempongeza mgombea kiti cha useneta kaunti ya Kisii, Okeng'o Nyambane kwa kufanikisha kutoa wimbo huo."Video bora zaidi ambayo nimefanya,Hongera seneta Okeng'o Nyambane" Embarambamba aliandika.