OMBI LA NDOA

Kwaheri! Selina hayumo tena sokoni

Mwigizaji mashuhuri Celestine Gachuhi amekubali ombi la ndoa la mwanamuziki Phil Kimemia siku chache tu baada kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari

•Mwigizaji mashuhuri Celestine Gachuhi amekubali ombi la ndoa la mwanamuziki Phil Kimemia siku chache baada kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa

•Wawili hao wamekuwa kwenye uhusiano kwa muda

Celestine na Kimemia
Celestine na Kimemia
Image: Hisani

Mwigizaji maarufu, Celestine Gachuhi, almaarufu kama Selina kutokana na mhusika anayecheza kwenye drama ya mapenzi ya Selina hayumo tena sokoni kwa wanaommezea mate baada yake kukubali ombi la ndo lake Phil Kimemia.

Celestine alikubali ombi la Kimemia ambaye ni mwanamuziki wa nyimbo za injili siku ya Jumapili. Kimemia alitoa ombi hilo siku chache tu baada ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Selina alitangaza kuwa alikubali kuolewa naye Kimemia kupitia ukurasa wake wa Instagram. Alichapisha picha ya mkono wake uliokuwa na pete na kuandika "Yes"(Ndio) chini yake ishara kuwa alikubali ombi la Kimemia kutaka ndoa. Wawili hao wamekuwa kwenye uhusiano kwa muda ila sasa wameamua kuifanya halali.

Wakenya wa tabaka mbalimbali haswa watu mashuhuri wameendelea kuwapongeza wawili hao huku wengine waliokuwa wanamtamani mwigizaji yule mrembo wakionyesha kuvunjika moyo kwao. Hizi hapa jumbe za baadhi ya Wakenya

Celestine hucheza kama mpenzi wake Pascal Tokodi almaarufu kama Nelson kwenye filamu ya Selina katika stesheni ya Maisha Magic East.