Jowie akata rufaa dhidi ya hukumu ya kifo

Jowie Machi 14 alihukumiwa kunyongwa na Jaji Grace Nzioka baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani.

Muhtasari

• Jowie anadai kuwa hukumu yake kuhusu mauaji ya Monica Kimani ilikiuka haki yake isiyoweza kupuuzwa ya uhuru kutoka kwa mateso na adhabu ya kikatili na ya kinyama.

, mshtakiwa wa kwanza katika mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani, katika Mahakama ya Milimani mnamo Februari 9, 2024. Picha: DOUGLAS OKIDDY
Joseph Irungu Jowie , mshtakiwa wa kwanza katika mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani, katika Mahakama ya Milimani mnamo Februari 9, 2024. Picha: DOUGLAS OKIDDY

Mfungwa wa mauaji Jowie Irungu ameiomba Mahakama Kuu akitaka hukumu ya kifo dhidi yake itangazwe kuwa ni adhabu ya kudhalilisha.

Jowie mnamo Machi 14 alihukumiwa kunyongwa na Jaji Grace Nzioka baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani.

Tayari amewasilisha notisi ya kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani kuhusu kutuhiwa na kuhukumiwa.

Katika ombi lake mbele ya Mahakama za Milimani, Jowie anasema njia ambayo hukumu ya kifo inapaswa kutekelezwa ni ya mateso, ukatili usio wa kibinadamu.

Anasema ni marufuku chini ya kifungu cha 25 cha katiba ambacho kinaelezea haki za kimsingi na uhuru ambao hauwezi kuwa na kikomo.

Mambo hayo yanatia ndani uhuru kutoka kwa mateso au adhabu ya kudhalilisha, uhuru kutoka kwa utumwa, na haki ya kuhukumiwa kwa usawa.

Jowie anadai kuwa hukumu yake kuhusu mauaji ya Monica Kimani ilikiuka haki yake isiyoweza kupuuzwa ya uhuru kutoka kwa mateso na adhabu ya kikatili na ya kinyama na anataka mahakama itamke hivyo.

Amemshtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika ombi lake.

Mnamo mwaka 2017, Mahakama ya Juu ilitangaza hukumu ya kifo ya lazima kuwa kinyume na katiba lakini haikuharamishwa.

Uamuzi huo ulimpa jaji uhuru kuamua ikiwa atatoa hukumu ya kifo au kifungo cha maisha.

Kutokana na hali hiyo, Jowie anaitaka mahakama itamke kuwa kifungu cha 379 (4) ni kinyume cha katiba kwa kuwa kinawanyima watu waliohukumiwa kifo haki ya dhamana wakati wa kukata rufaa.

Pia anataka afidiwe kwa sababu ya kukiukwa kwa haki zake.