"Hatukuwa marafiki na babangu!" Baha afunguka kutokuwepo kwa babake kulivyoathiri anavyomlea binti yake

Alifichua kuwa ingawa babake alikuwa akimpatia kila alichotaka, walikosa uhusiano kwani hakuwa naye.

Muhtasari

•Baba huyo wa binti mmoja alifichua kwamba alipokuwa mtoto, hakuwa na fursa ya kuwa karibu na babake.

•Alisema hafikirii kuondoka nchini Kenya kutafuta fursa bora zaidi kwani anataka kuwa karibu na bintiye zaidi.

Image: INSTAGRAM// TYLER MBAYA

Muigizaji na mtayarishaji wa maudhui maarufu wa Kenya Tyler Mbaya almaarufu Baha amefunguka kuhusu uzazi na jinsi maisha yake ya utotoni yalivyoathiri maisha yake  kama baba.

Akizungumza katika mazungumzo na The Dialogue Dive, baba huyo wa binti mmoja alifichua kwamba alipokuwa mtoto, hakuwa na fursa ya kuwa karibu na babake.

Alisema hillo ni jambo ambalo alitaka kufanya tofauti alipokuwa baba.

"Ubaba ni mzunguko. Wakati akikua, baba yangu alikuwa mbali kwa miaka kama 10. Sehemu kubwa ya utoto wangu, nilikua bila baba. Nikiget mtoto wangu nilisema hicho ndicho kitu cha kwanza nitakachojaribu, nikuwe tofauti kiasi with the psysical presence,” Tyler alisema.

Alifichua kuwa ingawa babake alikuwa akimpatia kila alichotaka, walikosa uhusiano kwani hakuwa naye.

"Baba yangu alikuwa akipanga kila kitu kinachohitajika. Alikuwa baba sahihi. Lakini ninahisi kama kuwa karibu na mtoto wako zaidi, unaweza kupata kuwa marafiki zao. Sidhani tulikuwa marafiki na baba yangu. Ilikuwa tu inakuja kutoka kwa heshima,” alisema.

Aliongeza, "Ndio uweze kuwa mzazi mzuri kwa mtoto wako, urafiki ni muhimu juu anakusikiliza kwa heshima na upendo, sio kwa woga. I feel like me trying so much to be in my kid’s life, naweza sema wale baba juhudi hiyo, sio rahisi . I appreciate other dads who make the step of being away, na hiyo pain anapitia kama vile kuwa karibu na mtoto wake, labda juu ya kazi ama mambo mengine. mapambano hayo ni kweli."

Muigizaji huyo wa zamani wa kipindi cha Machachari kwenye Citizen TV aliendelea kuzungumzia upendo wake mkubwa kwa bintiye na jinsi alivyojidhabihu kwa ajili yake.

Alisema hafikirii kuondoka nchini Kenya kutafuta fursa bora zaidi kwani anataka kuwa karibu na bintiye zaidi.

"Mashabiki wangu wote wanajua jinsi ninavyompenda mtoto wangu. Mimi niksema ni hadi my last breathe that I will be close to my kid, nitajaribu kila kitu. Ndio maana nilichagua kutoka kwenda ng'ambo kuhangaika. Ni chaguo, nimeona watu wanafanya hivyo lakini mimi niliona baba yangu akiifanya kitu hicho. Najua manufaa na madhara yake.

Mimi naweza sema kuwa karibu na mtoto wako ni kitu ambacho unapaswa kupigania. Kama inawezekana, ndiyo maana bado najaribu hapa. Ikiwa haiwezekani, ningekuwa huko Dubai. Nitaijaribu hapa nyumbani hadi itakapofanya kazi,” alisema.

Aliongeza, “Uzazi si jambo rahisi. Lakini ni safari ya kufurahisha, na ninaipenda kwa sababu ninajifunza upendo usio na masharti. Huyo mtoi nampenda bila kujali kama atanipenda, that’s a tough thing.