(Video) Je, Diamond kapata jiko? Akiri kupokea zawadi ya thamani kutoka kwa mkewe

Muhtasari

•Diamond alisema viatu vile vilikuwa zawadi aliyoletewa na mpenzi wake asiyejulikana kutoka nje ya Tanzania.

•Hata hivyo staa huyo wa muziki alikataa kufichua jina la mpenzi wake mpya huku akidai kwamba jina lake halipatikani hata kwa Google.

Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Image: INSTAGRAM

Je, Simba kapata windo lingine? 

Huenda nyota wa Bongo Naseeb Abdul Juma almaarufu kama Diamond Platnumz ana mke wa siri. Matamshi yake ya hivi majuzi alipokuwa anarekodi video ya wimbo 'Unachezaje' yamezua mjadala mkubwa mitandaoni iwapo mwanamuziki huyo amenyakua kipenzi kipya.

Katika video iliyoonekana na Radio Jambo, Diamond alionekana alionekana akionyesha kiatu cha thamani aina ya Bottega ambacho alisema kapokea kutoka kwa mkewe.

Diamond alisema viatu vile vilikuwa zawadi aliyoletewa na mpenzi wake asiyejulikana kutoka nje ya Tanzania.

"Hii Bottega original. Nimeletewa na mke wangu. Baby kaniletea kutoka sehemu tu. Hazitoka Tanzania, nje. Ni zawadi kutoka kwa mpenzi wangu. Bottega halisi!" Diamond alisikika akiambia wanahabari wa Wasafi Media.

Mwanamuziki huyo ambaye anaaminika kuchumbia ziadi ya wanawake 10 kutoka mataifa mbalimbali kufikia sasa alifichua kwamba viatu hivyo vilikuwa ghali mno.

Hata hivyo staa huyo wa muziki alikataa kufichua jina la mpenzi wake mpya huku akidai kwamba jina lake halipatikani hata kwa Google.

"Mimi singenunua, najijua. Kiatu ni ghali... hutapata kwa Google, hayuko pale" Diamond alisema.

Haya yanajiri wiki chache tu baada ya uvumi kwamba mwanamuziki huyo anachumbiana na malkia wa Bongo Zuchu kutanda kote.

Wawili hao walionekana pamoja katika hoteli moja ya kifahari nchini Tanzania katika hali iliyotiliwa shaka sana.

Hata hivyo Zuchu amejitokeza kudai kwamba hana mchumba kwa sasa na anasubiri mwanamume anayestahili.