Mwanamuziki Justina Syokau adai zawadi ya gari kutoka kwa 'crush' wake Ringtone Apoko

Muhtasari

•Hivi majuzi Justina alimsihi Apoko awache kuhangaika tena akitafuta mke huku akidai kwamba ako tayari kuolewa naye.

Justina Syokau// Ringtone Apoko
Justina Syokau// Ringtone Apoko
Image: INSTAGRAM

Hivi leo (Januari 13) mwanamuziki wa nyimbo za injili Justina Syokau anaadhimisha siku ya kuzaliwa kwake.

Mwanamuziki huyo ambaye alipata umaarufu mkubwa kutokana na kibao chake '2020' ataandaa hafla ya kusherekea siku hiyo maalum maishani mwake katika hoteli ya Swiss jijini Nairobi mwendo wa saa kumi jioni.

Justina amewaomba mashabiki wake kumtumia zawadi za siku ya kuzaliwa kupitia nambari yake ya simu.

"Heri ya kuzaliwa kwangu Utukufu kwa Mungu mwaka mwingine, ninamshangilia Yesu kwa mambo makuu aliyofanya Yesu unastahili nakupa sifa Zawadi zinawaelekeza katika nambari iliyo kwenye bango chini ya sherehe yangu ya kwanza ya kuzaliwa" Justina ametangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram

Kando na mashabiki wake Justina pia amemuomba mwanamuziki mwenzake Ringtone Apoko ampatie zawadi ya dhamani anaposherehekea siku ya kuzaliwa.

Justina ambaye hivi majuzi amekiri mapenzi makubwa aliyo nayo kwa Apoko amemsihi amnunulie gari aina ya Mercedes Benz.

"Hii ndio Aina ya Mercedes Benz ninayotaka ninaposherehekea siku yangu ya Kuzaliwa . Ringtone fanya Mambo yako😊 @ringtoneapoko" Justina aliandika na kuambatisha ujumbe wake na picha ya Mercedes yenye rangi ya maroon.

Hivi majuzi Justina alimsihi Apoko awache kuhangaika tena akitafuta mke huku akidai kwamba ako tayari kuolewa naye.

Justina alikiri kwamba Apoko ndiye mwanamume anayemezea mate zaidi nchini Kenya na angependa kuwa kipenzi chake.