Nikome!Aliyekuwa mpenzi wake Harmonize Frida Kajala amuonya Ringtone dhidi ya kumtumia jumbe

Muhtasari
  • Aliyekuwa mpenzi wake Harmonize Frida Kajala amuonya Ringtone dhidi ya kumtumia jumbe
Muigizaji Fridah Kajala
Image: Fridah Kjala/INSTAGRAM

Aliyekuwa mpenzi wake Harmonize, Frida Kajala kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram  amemuonya msanii wa nyimbo za injili nchini Ringtone dhidi ya kumtumia jumbe.

Kulingana na Kajala Ringtone amekuwa akimtumia jumbe pamoja na mwanawe Paula Kajala.

"Nikome kunitumia messages na kumtumia mwanangu Paula Kajala. Wanaume wa Kenya sijui ni nini mbaya na nyinyi," Frida Alisema.

Kajala amekuwa akigonga vichwa vya habari kuanzia mwaka jana baada ya kutangaza wazi kuwa ni mpenziwe Harmonize, ambapo uhusiano wao ulizua hisia tofauti mitandaoni, huku wawili hao wakiachana.

Wawili hao wanaonekana kila mmoja kuendelea na maisha yake baada ya kuachana.

Hii sio mara ya kwanza Ringtone kuwatamani watu maarufu wenzake, bai wamekuwa wakimkataa.