Mhubiri Mike Todd aomba washirika wake msamaha

Muhtasari

•Todd amejitokeza na kuomba msamaha kufuatia video yenye ilikuwa ikienea kwenye mitandao ya kijamii akiwa  kwenye madhabau.

•Alieleza kwamba ingawa Yesu aliweza kutumia mate yake kutenda mijiuza, kwa kipindi hiki hasa cha Corona alikosea kutumia mfano  aliotumia kwenye video hio,

Mike Toddi na mwanawe
Mike Toddi na mwanawe
Image: Instagram/mike toddi

Mhubiri Mike Todd ameomba msamaha kufuatia video ilikuwa ikitamba kwenye mitandao ya kijamii akiwa  kwenye madhabahu.

Kwenye video hio, Mhubiri huyo  alionekana kwenye madhabau  akitema mate kwenye kiganja cha mkono kisha kumpaka mshirika.

Todd alisema kwamba alikuwa anatumia tukio hilo kama mfano lakini alikuja kufahamu kwamba alikuwa amevuka mipaka katika mfano wake.

Alieleza kwamba ingawa Yesu alitumia mate yake kutenda miujiza, kwa kipindi hiki hasa cha Corona alikiri kuwa mfano  aliotumia kwenye video hiyo haukufaa, huku akikiri  ameelewa bayana madhara ya kutumia mfano huo na kuwaeleza washirika wake kwamba tukio hilo limekuwa funzo kwake na wachungaji wengine.

Kulingana naye tukio hilo ni la kusambaratisha ujumbe huo na kusema wakati ujao atatafakari upya mifano atayokuwa  anatumia katika mahubiri yake.