Nandy mjamzito? Mwijaku akana madai

Muhtasari

• Nandy amekuwa hivi majuzi akionekana akivaa nguo kubwa kubwa  kitu ambacho  si kawaida yake huku mashabiki wakitabiri kuwa msanii huyo ana ujauzito.

• Kwenye video hiyo, ambayo  Mwijaku alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram alionekana akishika malkia huyo tumbo lake na kuthibitisha  kuwa hana ujauzito wowote.

Nandy na Mwijaku
Nandy na Mwijaku
Image: Instagram/mwijaku

Baada ya uvumi kuenea kwenye mitandao ya kijamii kwamba  msanii wa Bongo Flava Nandy almaarufu The Afican Princess kwamba ana ujauzito.

Wandani wake hasa Mwijaku wamejitokeza na kutupilia mbali madai hayo.

Nandy amekuwa hivi majuzi akionekana akivaa nguo kubwa kubwa  kitu ambacho  si kawaida yake huku mashabiki wakitabiri kuwa msanii huyo ana ujauzito.

 Mwijaku alitumia kipindi ambacho msanii huyo alikuwa amealikwa kwenye kituo  kimoja cha habari  nchini Tanzania, kuweka bayana  mambo kwa kupuuzilia mbali madai kwamba Nandy anatarajia kufungua  na kuwaonya  wanaoeneza uvumi huo kukoma.

Kwenye video hiyo, ambayo  Mwijaku alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram alionekana akishika malkia huyo tumbo lake na kuthibitisha  kuwa hana ujauzito wowote.

"Na jambo nzuri zaidi  Nandy si mjamzito, watu mliosema Nandy ni mjamzito hapana, nimemguza kwa mkono wangu mimi, hana...ndugu yangu Bilyass unakwama wapi?" Mwijaku alisema kwenye video hiyo.