Romy Johs Mwandani wa Diamond amuomba Mulamwah Msamaha

Muhtasari

•Amejitokeza na kumuomba msamaha Mchekeshaji wa humu nchini Mulamwah.

•Mchekeshaji huyo aliibua madai kwamba picha yenye DJ Jons alitumia hakuwa na idhini kuitumia.

Image: INSTAGRAM// MULAMWAH

Mwandani wa Diamond tangu utotoni Romy Jons amejitokeza na kumuomba msamaha Mcheshi wa humu nchini Mulamwah.

Mchekeshaji huyo aliibua madai kwamba picha yenye DJ Jons alitumia hakuwa na idhini kuitumia.

Katika Picha hio, Mulamwah anaonekana akiwa hana shati huku kando yake akiwa na aliyekuwa mpenzi wake Carrol Sonnie akiwa amevalia vazi jeupe. Wawili hao walitalikiana mwezi jana.

Johs alitumia ukurusa wake wa Instagram kuchapisha picha hio huku ikiambatanisha na ujumbe uliokuwa unatangaza dawa za kuongeza nguvu za kiume.

"Ndugu yangu Romy Jons, tafadhali usitumie picha zetu kwa matangazo ya biashara bila ruhusa. Hasa mambo yanayohusiana na nguvu za kiume. Ifute. Mnatudhalilisha,” alisema Mulamwah

Baada ya habari hizo Romy Joh amemwandikia ujumbe kumuomba msamaha huku akiahidi kutoa picha hio.“Pole ndugu yangu. Acha niishushe,” aliandika