Labda kimakosa hakuna atakaye ona watoto wangu-Huddah Monroe atangaza

Muhtasari
  • Kwa muda Huddah amekuwa akiwasuta watu mashuhuri ambao wamekuwa wakiwapakia watoto wao mitandaoni kwa ajili ya umaarufu
Mwanasosholaiti Huddah Monroe
Image: Hisani

Mwanasosholaiti maarufu Huddah Monroe kwa sasa anafahamika sana na mashabiki wake kupitia kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa muda Huddah amekuwa akiwasuta watu mashuhuri ambao wamekuwa wakiwapakia watoto wao mitandaoni kwa ajili ya umaarufu.

Huddah ni mmoja wapo wa watu mashuhuri ambao huzungumza na kutangamana na mashabiki wao hasa kupitia kwenye itandao ya kijamii ya instagram

Amezua hisia tofauti mitandaoni baada ya kukiri kwamba hamna mtu yeyote ambaye atawaona watoto wake labda kimakosa.

"Maoni yangu mwenyewe,watoto wangu hakuna atakaye waona, hilo ni kwa MUngu labda kimakosa, kwanza watakuwa na kisha waamue kama wanataka kuwa kwenye huu mtego au la

Kwa sasa umetutega kabisa na hatuwezi kutoka,lakini tunaweza kuwalinda watoto wetu kutoka kwa huu mtego mbaya 

Unawea kuwaonyesha, lakini kuwafungulia akaunti na kadhalika, utakuwa umewaanika kabisa na hawataelewa watakapokuwa wakubwa," Huddah Alisema.