'Kienyeji yangu safi' King Kaka asifia mkewe, Nana Owiti

Muhtasari

•Jumatatu, siku ya wapendanao, King Kaka alitumia ukurusa wake wa instagram kueleza furaha isiyokuwa na kifani na kutaja Nana kuwa mwanamke anayemvumilia na kumpenda bila kero yoyote.

Nana Owiti na King Kaka
Nana Owiti na King Kaka
Image: INSTAGRAM// KING KAKA

Mwanamuziki Kennedy Ombima almaarufu King  Kaka amemsifia mkewe, Nana Owiti kwa kipindi  cha ndoa wamekuwa pamoja.

Ingawa kwa ndoa kuna changamoto chungu nzima, King Kaka alieleza kuwa Nana amekuwa akimpa motisha ya maisha kila wakati .

Jumatatu, siku ya wapendanao, King Kaka alitumia ukurusa wake wa instagram kueleza furaha isiyokuwa na kifani na kutaja Nana kuwa mwanamke anayemvumilia na kumpenda bila kero yoyote.

Vilevile, alimtania mke wake kidogo kwa kueleza kuwa kuna wakati huwa anamuudhi lakini kila wataki huwa mwenye kufungulia sura mpya ambayo humpa tumaini maishani.

"Mwandani wangu, Kienyeji yangu safi!, saa zingine huniudhi lakini mara nyingi hunifungulia sura mpya, Asante kwa kuwa hapa kila mara kwa ajili yangu na kwa hili. Kwa vile binadamu bado tunajifunza tafsiri halisi ya mapenzi, yangu ni Nana Owiti. Asante Mungu akubariki na hitaji la moyo wako litimie, nitakuwa hapa kukuongoza. Kila siku ni valentines," alisema King Kaka.