Wema Sepetu: Sijawahi kuomba mtu kunifanyia mchango

Muhtasari

•Aliwapongeza  mashabiki wake kwa kuonyesha upendo wakati wote huo ambao amekuwa kwenye tasnia ya uigizaji

•Alieleza kuwa kuchanga kwa mashabiki wake kulionyesha jinsi Watanzania wanamdhamini Muigizaji

 

Wema Sepetu
Wema Sepetu
Image: hisani

Muigizaji wa Filamu za Bongo Wema Sepetu ameeleza kuwa hajawai  kumwambia mtu yeyote kumfanyia mchango ili anunue gari.

Muigizaji huyo hata hivyo alisema kwamba waliomchangia walifanya hivyo kwa hiari yao wenyewe.

Akihojiwa kwenye kituo kimoja cha habari nchini humo, Sepetu alisema kuwa kuchanga kwa mashabiki wake kulionyesha jinsi Watanzania wanamdhamini.

"Mimi binafsi sikuwai kuomba mtu yeyote anichangie pesa, nadhani ilikuwa kuonyesha jinsi wanavyonipenda na watu wakaamua wafanye walichokuwa wakifanya lakini nilishawambia kwamba sipendi na wasitishe  michango. Na nina imani walisitisha, kusema ukweli sijui kilichoendelea kutoka hapo na sikutaka kujihusisha kwa sababu sijawai kutoka mwanzo kuomba pesa,"alisema Wema Sepetu.

Kauli ya Wema imejiri baada ya kuwa kimya  kutokana na maneno aliyoyasema  Aristostle kwamba ni muigizaji mashuhuri ambaye  hana gari la kifahari kama waigizaji  wengine.

Hata hivyo alikwepa kuzungumzia kauli hiyo,huku akitaja kuwa Aristostle alikuwa na nia mbaya ya kumdhalilisha kwa hivyo haikuwa na haja ya kujadili  kauli yake.

Vilevile aliwapongeza  mashabiki wake kwa kuonyesha upendo wakati wote huo ambao amekuwa kwenye tasnia ya uigizaji.