Romy Jons abaki hoi na emoji za Diamond kwa post ya Zuchu

Muhtasari

• Ndugu yake mkubwa na Diamond amebaki hoi baada ya kuona jinsi ambavyo msanii huyo anavyoachia maoni ya mapenzi kwenye post za instagram zake Zuchu.

Zuchu na Diamond
Zuchu na Diamond

Tetesi za mahusiano ya kimahaba kati ya msanii Diamond Platnumz na msanii mwenza Zuchu bado zipo hai muda mrefu baada ya dslili zote kuendelea kufichuka kwamba wawili hao huenda wako na mahusiano ambayo wameamua kuyaweka nyuma ya pazia.

Juzi kati hapa Zuchu alipakia picha zake nzuri tu kwenye ukurasa wake wa instagram na Diamond akaonekana pale akijiachia kwenye maoni na kumwaga ma emoji za mapenzi kama zote.

Hili liliwavutia watu wengi kwenye ‘comment’ hiyo yake ambayo wenye midomo waliitumia barabara kusema mengi kuhusu uvumi wa mapenzi kati ya Diamond na Zuchu.

Ila sasa kilicholeta mihemko zaidi ni wakati ndugu yake mkubwa wa Diamond, Romy Jons kuwa mmoja wa wachangiaji kwenye ile ‘comment’ ambapo alimtania Diamond Platnumz kwamba hayo makopakopa ambayo ameyamwaga kwa picha ya Zuchu ni mengi mno.

Haya makopa ni mengi sana mdogo wangu…” aliandika Romy Jons.

Wengine vwalizidi kumuambia Diamond hata akaficha vipi penzi ni kama kikohozi na kitatoka tu huku wengine wakimuambia mwezi mtukufu wa Ramadhan unakaribia na afanye kumuoa Zuchu wakati huo.