Mwandishi wa kitabu "How To Murder Your Husband" ashtakiwa kwa mauaji ya mumewe

Muhtasari

• Mwanmke huyo aliyetambulika kwa jina la Nancy Crampton-Brophy alichapisha kitabu mnamo mwaka 2011 kilichokuwa kinatoa mwongozo kwa wanawake wenza jinsi ya kuwaua wanaume wao na kukwepa bila kushtakiwa.

Nancy Crampton-Brophy, mwandishi aliyeua mumewe
Nancy Crampton-Brophy, mwandishi aliyeua mumewe
Image: ABC

Mwanamke mkongwe mwenye umri wa miaka 7 ambaye wakati mmoja aliwahi andika kitabu kuhusu jinsi ya kumuua mumeo amejipata taabani baada ya mahakama kumpata na hatia ya kumuua mume wake miaka kadhaa baada ya kuchapishwa kwa mswada huo wake.

Mwanmke huyo aliyetambulika kwa jina la Nancy Crampton-Brophy alichapisha kitabu mnamo mwaka 2011 kilichokuwa kinatoa mwongozo kwa wanawake wenza jinsi ya kuwaua wanaume wao na kukwepa bila kushtakiwa.

Nancy ambaye ni mchapishaji wa kujitegemea wa Makala yanayohusiana na huba na mahusiano ya kimapenzi alishtakiwa miaka saba baadaye kwa mauaji ya aliyekuwa mume wake Daniel Brophy aliyekuwa na umri wa miaka 63 kipindi hicho, ambaye alikuwa ni mpishi.

Mwandishi na mchapishaji huyo alishtakiwa kwa mauaji ya mumewe aliyepatikana amefariki katika jikoni nyumbani kwao na kupatikana na majeraha ya risasi mgongoni na kifuani pake ambapo mwanamke huyo bila woga alichukua katika mitandao ya kijamii kutangaza kifo chake.

Baada ya kutiwa nguvuni kulingana na vyanzo vya habari nchini Marekani, uchunguzi wa kina umefanywa kwa takribani miaka minne sasa ambapo Nancy amepatikana na hatia ya mauaji ya mumewe kwani hakuna mtu mwingine tena aliwahi tiwa mbaroni kutokana na mkasa huo uliotokea jikoni mwao.