Baadhi ya masuala katika maisha ya Vishy akifikisha miaka 21

Alisema siku hii itakua ya aina yake, siku ya kukata na kisu kikali.

Muhtasari

• Pritty Vishy alipata umaarufu kwenye mitandao ya kijamii baada ya  kuweka wazi mahusiano ya kimapenzi na msanii Stevo Simple Boy.

• Alifichua kuwa Stevo Simple Boy alishindwa kuhudumia mahitaji ya mwili wake hivyo kuishia kupata faraja sehemu nyingine ndiposa akamwacha.

Mwanablogu asherehekea siku yake ya kuzaliwa
Pritty Vish Mwanablogu asherehekea siku yake ya kuzaliwa
Image: Facebook

Oktoba 3 ,2022, Pritty Vishy mwanasosholiti tajika humu nchini alisherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Mwanamitindo huyu ambaye alizaliwa na kulia mjini Nairobi, sasa anafurahia kufikisha umri wa miaka 21. Siku ambayo alisema itakuwa ya aina yake, Siku ya kukata na kisu chenye makali kuwili.

Pritty Vishy alipata umaarufu kwenye mitandao ya kijamii baada ya  kuweka wazi mahusiano ya kimapenzi na msanii Stevo Simple Boy.

Mwanamuziki Stevo Simple Boy ambaye walichumbiana na mwishowe kuachana, walikandiana vikali na kukunjiana mashati kwenye mitandao ya kijamii huku kila mmoja akilichafua jina la mwenzake ili kupata umaarufu mitandaoni humo.

Kulingana na Pritty Vishy alifichua kuwa Stivo Simple Boy alishindwa kuhudumia mahitaji ya mwili wake hivyo kuishia kupata faraja sehemu nyingine ndiposa akamuacha.

Baadaye msanii Stevo Simple Boy maarufu kwa kibao cha ‘Freshi Barida’ alitangaza kwamba amepata mchumba na hata kumvisha pete hadharani.

Mwanablogu Vishy naye aligeuka mjadala kwenye mitandao ya kijamii wakati alipomjibu shabiki wake mmoja aliyetaka kujua idadi ya wanaume ambao wamekuwa katika uhusiano. 

Mwanadada huyu aliwashangaza wengi alipotangaza ameshiriki uhusiano wa kimapenzi na takribani wanaume 10 au 15 idadi ambayo hana uhakika nayo.

Kando na hayo, majuma kadhaa yaliopita Vishy alikiri kwamba huwa anavutiwa na wanawake wenzake kwani alisema kwamba  huwa  anapandwa na hisia  anapowaona wanawake waliobarikiwa upande wa makalio.

Alisema aliwahi kutongozwa na mwanamke shoga ambaye waliishia katika mahusino hadi kutumiana picha na video.

“Mi nishawai, ata achana picha hadi video. Ilikua dem mwingine tulikutana na yeye Facebook alikua lesbian. Nilikua eager kujua les wanafanyanga nini si tukaslide hadi WhatsApp akanitumia nudes zake akaniambia  nitumie zangu pia na mi nikamtumia hadi video,” Pritty Vishy alisema.