Mwanamuziki Akothee aweka wazi thamani yake

Akothee alisema kuwa thamana yake kubwa ni watoto wake

Muhtasari

• "Nina vyeti vya kuzaliwa vitano chini ya jina langu,"mwanamuziki huyo aliwaambia mashabiki wake.

Akothee

Mwanamuziki Akothee ameweka wazi thamani yake baada ya wanasiasa kufichua thamana zao na watu kumuuliza.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Akothee alisema kuwa thamani zake ni tano ambayo  ni mambo muhimu sana katika maisha yake.

Alisema kuwa thamani yake kubwa ni watoto wake watano wenye baba tofauti tofauti.

Alifafanua zaidi na kutaja jinsia za watoto wake, wawili wa kiume na mabinti watatu ambao sasa ni watu wazima.

"Nina vyeti vya kuzaliwa vitano chini ya jina langu,"mwanamuziki huyo aliwaambia mashabiki wake.

Mwanamuziki huyo amekuwa akijivunia kuwa mama ya watoto watano na hata kuzuru nchi mbali mbali nao.

Aliwalea na kuwasomesha watoto wake na hata kuwalipia karo katika shule za kifahari ili waweze kuwa na mafanikio ya mbeleni.

Mama huyo wa watoto watano alifichua kuwa alitumia takriban shilingi milioni kwa masomo ya chuo kikuu ya binti yake, Fancy Makadia.

Alisema pia kuwa yeye huwa halipi karo moja kwa moja hadi shuleni na kuwa alikuwa akiwatumia mabinti wake pesa hizo.

Nilituma pesa  kwenye Akaunti yake, kwa hivyo alikuwa na chaguo la kununua maisha yake ya baadaye au kutumia pesa na kuanza kulaumu kila mtu," Akothee alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Mabinti wote wa Akothee wamesoma hadi chuo kikuu.

Watoto wawili wa mwisho wa mwanamuziki huyo wanasomea Ufaransa ambapo wanaishi na baba ya mtoto wake wa mwisho.