(+video) Mwanamke wa miaka 40 alalamika kuhusu ugumu wa kupata mpenzi

Mwanamke huyo alisema hafurahishwi na upweke uliomwandama kwa muda mrefu.

Muhtasari

• Mwanamke huo alilalamika kwenye mitandao ya kijamii akijidai kwamba ana umri wa miaka 40 na bado hajapata bwana.

•Mwanadada huyo alisema anamwomba Mungu sana siku moja amjalie na mwanamume mmoja ambaye atampa huba.

Mwanamke alalamika kukosa bwana wa kumuoa
Mwanamke alalamika kukosa bwana wa kumuoa
Image: TikTok//@user5541238600873

Mwanamke mmoja  aligeuka gumzo la siku baada ya kuonekana akilalamika kwenye mitandao ya kijamii akijidai kwamba ana umri wa miaka 40 na bado hajapata bwana.

Kupitoa Tiktok, mwanamke huyo alisema hafurahishwi na upweke uliomwandama kwa muda mrefu na kubainisha kuwa maisha yake hayaendi shwari jinsi  ipasavyo.

Kwenye video ambayo alipakia alionekana akiwa amezama kwenye bahari la mawazo na kudai hana watoto ila anatumai kuwa ataolewa siku moja.

Mwanadada huyo alisema anamwomba Mungu sana siku moja amjalie na mwanamume mmoja ambaye atampa huba.

Miaka 40 sasa, sina watoto, mume au kwenye mahusiano wowote. Mungu wangu nisaidie,'' Mwanamke huyo aliomba akionyesha masikitiko yake.

Video hiyo iliwagusa moyo sana watu walioitazama  huku wakionyesha kumpa matumaini kwamba siku moja atapatana na mume atakayempenda si kiasi.

Lina Lina66158: "Usikate tamaa mwanadada, nilikuwa na rafiki yangu alikuwa na miaka 48. na Mungu alimfanyia muujiza. sasa ameolewa na ana watoto wawili." 

Agmadalo2: "Usikate tamaa dada yetu, Mungu yupo na wewe, wakati wa Mungu ni bora zaidi."

Lawon9676yolo: "Mwenyezi Mungu atayafuta machozi yako na ataitimiza haja ya moyo wako."

Secure the bag:  "Neema ya kuzaa ikupate dada yetu. Mungu mwenye uwezo yupo nawe."