(+video) "Walisema singefika miaka 15, sasa niko na miaka 25" Mwathirika wa Sickle Cell asimulia

Alisema kwamba madaktari walimshauri mama yake kupata mtoto mwingine kwani yeye alikuwa wa kufa tu!

Muhtasari

• Mmeona mrembo ambaye ni shujaa wa kupigana na ugonjwa wa seli mundu? Na ni kweli, ninafikisha miaka 25 Novemba 7. - alieleza.

Mwanadada mmoja kupitia mtandao wa TikTok amewaliza wengi baada ya kupakia video yake ya kutoa shukrani kwa Munu katika kile alisema kuwa ni kupata uponyaji kutokana na ugonjwa ambao wengi walimdhihaki kwam a hangepata tiba.

Mwanadada huyo kwa jina Sireonit alisema kwamba anaugua ugonjwa wa seli mundu kwa kimombo Sickle Cell Anaemia na kutokana na athari za ugonjwa huo lakini pia na dhana zinzzohusishwa nao, wengi walikuwa wakifikiria kwamba hangeishi kwa muda mrefu.

Akielezea hadithi ya maisha yake kupitia TikTok, Sireonit alisema kwamba mamake alipoambiwa kwa mara ya kwanza kuwa binti wake alikuwa ameathirika na ugonjwa wa seli mundu, madaktari walimuusia kuwa hangeishi zaidi ya miaka 15. Madaktari hao pia walimshauri mama mtu kujipanga kupata mtoto mwingine kwani huyo mwisho wake ungekamilika tu pindi atakapofikisha miaka 15.

Mwanadada huyo alijivunia uwepo wa Mungu katika maisha yake kwa kusema kwamba alivunjilia mbali dhana hizo na kudokeza mnamo Novemba 7, atasherehekea kufikisha miaka 25 akiwa hai na pia mwenye mafanikio makubwa, miaka 10 juu ya ile ambayo waimwengu walikuwa wamemtabiria kifo.

“Mmeona mrembo ambaye ni shujaa wa kupigana na ugonjwa wa seli mundu? Na ni kweli, ninafikisha miaka 25 Novemba 7. Waliambia mamangu kuwa ningeishi kwa miaka 15 tu na kumtaka azae mtoto mwingine,” Mwanadada huyo aliandika kwenye video ile.

Alisema kuwa kando na kupindua utabiri wa walimwengu, pia amefanikiwa na kuwa nesi ambaye amemfanya mamake kujihisi wa kujivunia mafanikio yake pakubwa.

“Tafakari nani anampendezesha mama leo, ndio ni mimi, nesi ambaye pia anaendesha biashara ya nguo pamoja na wakfu wa kuwatia moyo watu wenye hali kama yangu, niite tu mjasiriamali,” mwanadada huyo alijivunia.