"Nataka kuwa nawe" Shakib ajawa bashasha baada ya mpenzi wake Zari kumsherehekea

Mpenziwe Zari aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa siku ya Jumatatu.

Muhtasari

•Shakib ambaye ni maelezo yake machache tu yako hadharani alisherehekewa kutimiza miaka 30.

• Huku akimsherehekea, mwanasoshalaiti huyo alimtambulisha Shakib kama mfalme wake.

Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Mpenzi wa mwanasoshalaiti maarufu Zari Hassan, Shakib Cham Lutaaya aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa siku ya Jumatatu, Desemba 5.

Shakib ambaye ni maelezo yake machache tu yako hadharani alisherehekewa kutimiza miaka 30.

Huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, Shakib Cham alichukua fursa kuwatakia watu barua maishani.

"Siku yako ya kuzaliwa ibadilishe chuki yote kuwa upendo, kutofaulu kuwa mafanikio, adhabu zote kuwa baraka na vizuizi vyote kuwa fursa. Nakutakia siku njema ya kuzaliwa🎁🎂🎈," alisema kwenye Instagram.

Makumi ya wanamitandao walimiminika chini ya ujumbe huo wake kumsherehekea na kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zari alimsherehekea mpenzi huyo wake na kumtakia baraka maishani. Huku akimsherehekea, mwanasoshalaiti huyo alimtambulisha Shakib kama mfalme wake.

"Kheri ya siku ya kuzaliwa mfalme K, Hapa kukutakia siku njema ya kuzaliwa na baraka nyingi zaidi maishani 💞," Zari alimwandikia mpenziwe.

Mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz aliambatanisha ujumbe wake na picha zake kadhaa na kipenzi hicho chake.

Shakib ambaye alishindwa kuzuia msisimko wake mkubwa kufuatia ujumbe huo alijibu kwa kusema anatamani Zari awe mpenziwe wa maisha.

"Picha nzuri za Sisi 😍💕 Nataka kuwa nawe 🤗❤️😁," alisema.

Jumatatu, Shakib, ambaye ni raia wa Uganda, alipakia picha akiwa ameketi juu ya gari jipya kabisa la manjano aina ya Jeep huku akijisherehekea kwa kuona mzunguko mwingine mpya wa maisha yake.

Mpenzi wake Zari aliungana na wanamitandao wengine kumpongeza kwa kujipatia zawadi hiyo ghali.

“Heri ya siku ya kuzaliwa mpenzi wangu na pongezi kwa gari jipya🚘❤️🙌. Baraka zaidi babe💓” alimwambia.

Zari alimtambulisha Shakib kama mpenzi wake mpya mapema mwaka huu baada ya kutengana na mfanyibiashara wa Uganda GK Choppa. Hapo awali aliwahi kuwa na ndoa na Ivan Semwanga na Diamond.