Najivunia kuwa shoga -Jude Magambo asimulia

Napenda mapenzi ya jinsia nimeyafanya kwa muda mrefu

Muhtasari

•Nimekuwa nkifanya mapenzi ya njinsia moja kwa muda mrefu, ikafika wakati watu wengi wakaanza kunishuku nami nikachukua jukumu la kujitokeza kwa umma mbila kuogopa kwa sababu singeendelea kuficha zaidi kwa maana najivunia kuwa shoga

Jude Magambo mwanaume anayejitambulisha mara nyingi kama Manze wa Meru ameshangaza wengi kwa kujivunia kuwa shoga ambaye hujitambulisha kwa mitandao bila hofu.

Kwenye mahojiano na mwanablogu Nicholas Kioko,Jude Magambo  ambaye hapendi kutambuliwa kama mwanaume mara nyingi hujitokeza kwa umma na mavazi ya kike.

"Nimekuwa nafanya mapenzi ya njinsia moja kwa muda mrefu hadi ikafika wakati watu wengi wakaanza kunishuku nami nikachukua jukumu la kujitokeza kwa umma mbila kuogopa kwa sababu singeendelea kuficha zaidi".Jude Magambo alisema.

Baada ya mwanablogu Nicholas Kioko kutaka kujua zaidi kuhusiana na mapenzi haya ya jinsia moja Jude Magambo alisimulia zaidi .

"Napenda sana jinsi nilivyo kuwa na mapenzi ya jinsia moja mimi ndio utumika kama mwanamke ndio maana napenda kutumia jina la manze wa Meru,kwa watu wengi hawapendi jambo ambalo nafanya lakini kwangu najivunia sana ni jambo zuri na nalipenda zaidi '.Jude alisema.

Alidhibitisha pia uhusiano wake na mwana Tiktoker Brian Chira akikataa madai ya kuwa pamoja ndani ya usiano wa  mapenzi ya njinsia moja.

"Mimi na Brian Chira tulikuwa tu marafiki na kufikia wakati huu sisi si marafiki tena ,alikuwa tu rafiki yangu nilimsaindia tu  kama rafiki wakati mwingi alikuwa kwa shinda nilisimama naye kwa kila jambo"...wakati mwingi nilimuomba awache kumbugia pombe . Magambo alisimulia.